Kwa mjibu wa
msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso
mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja kama Komba ameshakamatwa kuhusiana na
kuwepo mtandao mkubwa ndani na nje ya jeshi hilo unajiusisha na
kuwalaghai vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi.
Inasemekana vijana zaidi ya 200 walitapeliwa kiasi cha shillingi
800,000/= kila mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha kujiunga na Chuo cha
Polisi Moshi baada ya kuhonga kitita hicho walitakiwa kulipa tena
25,000/= kama nauli ya kuwafikisha Moshi na kweli mabasi matatu
yalikodishwa nakuwafikisha Moshi chuoni.
Baada yakufika chuoni taratibu zote za kuwasajili pamoja na kutakiwa
kulipia gharama nyingine za kiasi cha shillingi 50,000/=,walinyolewa
vipara na kuanza kupiga kwata kama makuruta wengine.
Kwa mshangao wa vijana hao siku ya pili waliitwa nakuambiwa kuwa
wanatakiwa kuondoka hapo chuoni kwa vile sio makuruta halali na hawako
kwenye kompyuta za chuo.
Kilichowashangaza zaidi ni pale walipokuwa wanatoka kweye lango la chuo
kurudi makwao waliyaona mabasi yale yale yaliyowaleta yakiingia na
vijana wengine ambao bila shaka nao wlikuwa wameingizwa mkenge!.
Msemaji wa Polisi ameamewataka wote wenye malalamiko au taarifa kuwa
walitoa fedha ili kupatiwa ajira na matapeli hao au mawakala wao kutoa
ushirikiano utakaowezesha polisi kukamilisha uchunguzi na kupata
ushahidiwa kudhibitisha kesi ya Komba iliyopo mahakamani.
Taarifa zitumwe kwa ujumbe wa mfupi kwa ssimu ya IGP namba 0754785557 au
kuwasiliana moja kwa moja makao makuu ya Polisi ghorofa namba 4 Ofisi
ya Malalamiko.
No comments:
Post a Comment