SUMATRA WATANGAZA BEI MPYA ZA NAULI YA DARADARA!!!!
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi
Kavu na Majini SUMATRA imetangaza
viwango vipya vya nauli za mabasi ya
masafa marefu, daladala katika jiji la Daresalaam,nauli za usafiri wa reli ya kati na bandari.
Viwango hivyo vimetolewa kutokana na
SUMATRA kufuatia maombi rasmi kutoka
kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na
makampuni binafsi nchini kutokana
ongezeko la gharama za uendeshaji.
Ahmad Kilima ni Kaimu mkurugenzi mkuu
wa SUMATRA amesema viwango vipya
vimetolewa baada ya kufuata taratibu za
kisheria na utendaji kwa kuwashirikisha
wadau mbalimbali katika kujadili na kupata maoni yao kuhusu ongezeko la nauli.
Amesema SUMATRA imeongeza viwango
vya juu vya nauli ya daladala kwa wastani
wa asilimia 24.46 na mabasi ya masafa
marefu viwango vimeongezwa kwa asilimia 20.3,Pia amesema ili kuhakikisha
kuwa kuna uwiano kati ya viwango vipya vya nauli na ubora wa huduma ya
usafiri, mamlaka imeewataka wamiliki wa mabasi kutotumia wapiga debe
katika kuuza tiketi za usafiri na kwamba watakaokaidi hatua za kisheria
zitachukuliwa.
Bwana Kilima amesema katika kufanya
mapitio ya gharama mbalimbali za bandari za bahari kuu mamlaka imeridhia
ongezeko la gharama kwa wastani wa asilimia 34.3 hivyo TPA wametakiwa
kuboresha huduma kwa wateja kwa kuanzisha kitengo cha huduma kwa wateja .
Hata hivyo ongezeko hilo la nauli limeenda sanjari na viwango vya nauli
kwa usafiri wa abiria wa reli ya kati ambapo mamlaka imewataka abiria
kukata tiketi na kupanda treni wakionyesha vitambulisho…
Viwango vipya vya nauli vinatarajia kuanza
kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili 2013
ambapo nauli ya mwanafunzi itakuwa
shilingi 200 na mtu mzima atalipa shilingi
400 kwa safari za mijini.
Maoni ushauli tuandikie bpromas@outlook.com.
No comments:
Post a Comment