JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru
mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa
kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya
vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.
Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi
baada ya masister wenzie kubaini kama si mmoja wao, kutokana na
kushindwa kufanya baadhi ya masuala ambayo ni msingi wa utawa wao.
Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa
Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila laKe ni Muwembu wa
nchini Kenya amekamatwa katika nyumba za masista zilizopo Ipogolo
mjini Iringa.
Aidha Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa
maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi
walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya
ndani na nje ya nchi.
Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za
kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye
namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba
A. 1790366.
Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea
nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi
karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.
Sister huyo FEKI amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye
ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia
vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya
kuingia humu nchini.
Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na wageni mbalimbali, huku
akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa muonekano wao, kutokana na
mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya kila mtu kumuamini.
HII NDO TAARIFA YA POLISI KUMUHUSU SISTER FEKI. |
HUYU NDO MTUHUMIWA ALIEKUWA ANAJIFANYA SISTER. |
No comments:
Post a Comment