Mabondia hao ni Case Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa na Petro Charles Mtagwa.
Wakati kesi hiyo ilipoanza
kusikilizwa, wote walikiri makosa ya kuingiza mihadarati hiyo nchini
Mauritius wakati walipokwenda kushiriki mashindano ya ndondi barani
Afrika mwaka 2008.
Wakiwa mbele ya Jaji, waliiambia mahakama kuwa
walilazimika kuingia katika biashara hiyo haramu kutokana na hali zao za
maisha kuwa maskini.
"Tunaomba radhi kwa taifa la Mauritius", waliiambia mahakama.
"Tu watu maskini na tunategemewa na familia, watoto na wazee wetu wanaotugemea."
"Kwa dawa hizi tungepata kiasi cha Pauni £4,000". walisema
Jaji Benjamin Marie Joseph alisema katika kutoa
adhabu hiyo yote hayo ameyafikiria, kwani walitoa ushirikiano mzuri
wakati wote wa uchunguzi wa kesi hiyo, kulikowezesha hata
wafanyabiashara hiyo, raia wa Mauritius kukamatwa.
Wamekuwa mahabusu kwa siku 1,722, sawa na miaka
miatano, hivyo watatumikia miaka kumi iliyobakia jela. Pia watatakiwa
kulipa faini ya pauni £1,600 na gharama nyingine za uendeshaji wa kesi
hiyo.
Jaji aliwashutumu kwa kuukosea
umma wa Mauritius kwa kuingiza dawa hizo za kulevya aina ya heroin.
Mabondia hao waliwasili Mauritius tarehe 10 Juni
2008 na kuweza kupita uwanja wa ndege bila kunaswa hadi walipokamatwa
katika hoteli waliyofikia ya Quatre Bornes.
Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.
|
No comments:
Post a Comment