Tuesday, June 25, 2013

GAZETI LA MAREKANI LAFICHUA ULINZI WA OBAMA UTAKAVYOKUWA AKIWA TANZANIA.

Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post Vyombo vya usalama vya Marekani vimejipanga kuhakikisha ziara ya kiongozi huyo haivurugwi kwa namna yoyote ile. Tayari ndege za jeshi zilizobeba magari ya akiba 56, yakiwemo 14 aina ya ‘Cadillac One’ maalumu kwa ajili ya kiongozi huyo, yamewasili katika nchi hizo tatu za Afrika atakazotembelea.

Kwa mujibu wa gazeti ilo  Ndege hizo pia zimebeba malori matatu ambayo yamesheheni karatasi maalumu za kuzuia risasi kupenya kwenye vioo, zitakazobandikwa kwenye madirisha ya hoteli ambazo Rais Obama na ujumbe wake watafikia.

Taarifa zinazidi kutanabaisha kuwa, mamia ya mashushushu wa Marekani tayari wako katika nchi hizo. Meli maalumu za kubeba Ndege za kivita, maarufu kwa jina la ‘amphibious ship,’ ikiwa na hospitali maalumu na yenye vifaa vyote itaweka nanga baharini, jirani na nchi atakayokuwa Rais Obama, tayari kukabiliana na dharura yoyote itakayotokea. Gazeti hilo liliandika kuwa ndege za kivita za Marekani zitakuwa zikipeana zamu kufanya doria kwa saa 24, katika anga la nchi ambayo Rais Obama atakuwepo, iwapo ndege za ‘adui’ zitakaribia eneo linaloitwa ‘anga ya rais.’ Kwa mujibu wa gazeti hilo, ziara ya Rais Obama aliyoifanya hivi karibuni katika nchi za Ujerumani na Ireland Kaskazini, japo kulikuwa na gharama kwa walinzi, lakini safari za nchi za Afrika zimeelezwa kuwa na gharama kubwa zaidi.

Tahadhari

Pia wameshauliwa ili kujikinga na ugonjwa wa malaria nchini, ujumbe wa Obama umeshauriwa kutumia dawa ya mbu ya kupaka na kupuliza inayoitwa Deet.

Juzi alipokuwa katika ziara nchini Ujerumani Wananchi wa nchi hiyo walishangaa kuona ulizi mkali sana kwa rais huyo uliokuwepo wakati akiwa nchini Ujerumani na wachambuzi wa maswala ya kiusalama wanasema kwa ziara yake kwa nchi za Afrika inayoanza mwishoni mwa wiki hii ulinzi utakuwa zaidi ya ulivyokuwa nchi ya Ujerumani. 

 Habari hii iliandikwa na mtandao mmoja nchini Ujerumani kuhusu ulinzi wake

Berlin Ramps Up Security for Obama Visit

 The square facing the Brandenburg Gate, Pariser Platz, will be closed to normal traffic for an entire week, beginning on Friday. And Berlin will be under the highest security level, 1+, according to the news agency DPA, which involves snipers on rooftops, sealed-off manhole covers, bomb-sniffing dogs, numerous street closures and larger security zones.


No comments:

Post a Comment