Tuesday, June 18, 2013

MAMBO YAANZA KUIBUKA ARUSHA MTOTO ASEMA "ALIENIPIGA RISASI NI POLISI".

Mtoto Abubakar Adam (pichani) alisema  kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto.

Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini.

“Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi.

Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.

“Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni risasi au la,” alisema Semdeli.(Habari hii kwa msaada wa Gazeti la mwananchi laTanzania.)


No comments:

Post a Comment