Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja
kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa
Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha
kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za
kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi
yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini
Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza
kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika
watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George
Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na
Jumatano ijayo.
“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa
hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na
kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za
kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la
litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni
hao.”
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo,
baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi
na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na
ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia
wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.Wasafiri
wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama
atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion
Ubungo.
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa
4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa
mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na
wakati huo.
Sasa kutokana na kauli hii ule msemo wa Mgeni njoo mwenyeji...........tuubadilishe na iwe Wageni njooni wenyeji......... Tupe maoni yako hapa bpromas@outlook.com
No comments:
Post a Comment