|
Baadhi ya Ndugu wa Familiya ya Mzee Nelson Madela wakibeba mabaki ya mwili wa mtoto wake kuurudisha katika eneo lililoamliwa na Mahakama.
|
|
Msafari ukielekea Eneo la Qunu ambapo ndipo mabaki ya miili hiyo ya watoto wa Nelson madela yanazikwa upya kwa amli ya mahakama.
|
|
Mtoto wa NELSON MANDELA Makiziwe Mandela ( katikati) akielekea kwenye Gari baada ya Maziko ya Ndugu zake katika Eneo la Qunu.
|
|
Mandla Mandela mjukuu wa Rais wa zamani wa A frika Kusini pamoja na Mama yake Nolusapho Mandela wakiongea na waandishi wa habari baada ya mahamuzi ya mahakama kutolewa.
|
Mabaki ya miili ya watoto watatu wa Mandela ambao ni
marehemu ilizikwa upya katika eneo la Qunu, yakiwa ni mazishi
ya mara ya tatu tangu walipofariki dunia katika vipindi tofauti, ukiwa
ni utekelezaji wa amri ya Mahakama Kuu ya Eastern Cape.
Uamuzi huo ulimaanisha kushindwa kwa mjukuu wa
Mandela, Mandla ambaye jana katika mkutano wake na waandishi wa habari
alisema: “Sikusudii kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama,” lakini
akahusisha ugomvi katika familia ya babu yake kwamba ni vita ya fedha na
mali za Mandela.
Mabaki hayo ni ya mtoto wa kwanza wa kiume wa
kiongozi huyo, Makgato aliyefariki dunia 2005, binti yake wa kwanza
Makaziwe (mkubwa) ambaye alifariki akiwa mchanga mwaka 1948 na mtoto
wake wa pili wa kiume, Madiba Thembekile aliyefariki katika ajali ya
gari 1969.
Mahakama Kuu ya Eastern Cape ilitoa uamuzi
uliowapa ushindi wanafamilia 16 wa Mandela ambao walifungua madai
wakiongozwa na shangazi yake Mandla, Makaziwe.
Jaji Lusindiso Pakade katika hukumu yake, mbali na
kutoa amri hiyo alitaja vitendo vya Mandla kuwa ni vya aibu visivyo vya
kibinadamu hivyo kutoa amri ya kufukuliwa miili hiyo na kisha
kurejeshwa Qunu. Mabaki hayo yalihamishwa kutoka kijiji cha Mvezo ambako
yalizikwa mara ya pili kwa kificho miaka miwili iliyopita na mjukuu
mkubwa wa Mandela, Mandla ambaye pia ni kiongozi wa kimila katika kijiji
hicho.
Kazi ya kufukua makaburi ya watoto wa Mandela
katika eneo la Mvezo ilifanyika hadi juzi usiku chini ya ulinzi wa
polisi baada ya madalali wa mahakama kutumia sururu kuvunja lango (geti)
kuu la kuingia katika makazi ya Mandla.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa eneo hilo,
Luteni Kanali Mzukisi Fatyela, uchimbuaji wa makaburi ulifanywa na
wataalamu wa Kituo cha Afya cha Mthatha na baadaye kupelekwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha kituo hicho juzi usiku na jana asubuhi
mabaki ya marehemu hao yalifanyiwa uchunguzi wa kimaabara kabla ya
kupelekwa Qunu kwa maziko.
No comments:
Post a Comment