JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA WANANCHI
Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa,
wanaoonekana katika hizi picha, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo
vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi
yetu. Jeshi
la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi
mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana
katika kituo chochote cha Polisi kilicho KaribĂș, ili waweze kukamatwa na
kufikishwa kwenye mkondo wa sheria. Ndugu
mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa
kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote
atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57. JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA WANANCHI
No comments:
Post a Comment