Taarifa za ndani kutoka Wizara ya Fedha zinasema kwamba Serikali
haina fedha kwa sasa ambapo sasa inalazimika kukusanya fedha kutoka
katika mashirika yake ili kuendesha shughuli zake.
Miongoni mwa mashirika ya umma yanayoguswa na
uamuzi huo wa Serikali ni mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwamo NSSF, PSPF,
Mamlaka Udhibiti wa Nishati na Maji(Ewura)Shirika la Ugavi wa Umeme
(Tanesco), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na mengine kadhaa.
Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti,
baadhi ya wafanyakazi wa Idara za Fedha za mashirika hayo, walieleza
kuwa kutokana uamuzi huo wa Serikali sasa wanalazimika kukaa ili kuandaa
upya bajeti za mashirika hayo.
“Ukweli haya maagizo yana athiri kubwa kwetu kwani
tayari tulikuwa tumepanga bajeti kutokana na mapato na kwa uamuzi huu
ambao kimsingi hakuna mamlaka ya kuyapinga, itabidi tutoe, ila adhari
zitakuwepo,”alisema ofisa mmoja wa juu wa moja ya mashirika ya umma.
Hata hivyo, alisema kuwa iwapo wangeshauriwa
mapema basi walau wangetakiwa kuchangia asilimia tano kwa mwaka huu wa
fedha na mwaka ujao ndipo ingeongezeka kufikia asilimia 10.
Ofisa mwingine wa shirika la umma aliyeomba
kutotajwa jina alieleza kuwa uchangiaji huo, ulipaswa kutazama
mashirika, kwani yapo yanayojiendesha kwa hasara, mengine yanapokea
ruzuku na mengine yanajiendesha kwa fedha zake.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumamosi umebaini kwa
Tanapa pekee inatakiwa kulipa Sh24 bilioni, zinazotakiwa kukatwa kutoka
kwenye bajeti yao ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya shirika na jamii
inayowazunguka.
Ukitaka kujua zaidi soma Ripoti hii ya Uchunguzi iliofanywa na Gazeti la Mwananchi.
|
No comments:
Post a Comment