Hawa ni baadhi ya wafanyakazi wa ndani walipokuwa katika mafunzo ya njisi ya kutoa huduma zao mahara pao pa kazi mafunzo hayo yaliratibiwa na AAR kwa udhamini wa CRDB. |
Wakifundishwa somo la kuhudumia watoto na Dr Kissah kutoka AAR. |
Mshahara wa watumishi wa ndani, sasa umewekwa kisheria kuanzia Julai mosi, kupitia tangazo la Serikali la Kima cha Chini cha Mshahara wa Kisekta, lililotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema.
Kwa
mujibu wa tangazo hilo lililochapishwa jana katika vyombo vya habari,
wafanyakazi wote wa ndani walioajiriwa, mbali na wanaofanya kazi za
ndani kwa makubaliano mengine yasiyo ya ajira, kama muda mfupi na
kuacha, wanapaswa kulipwa si chini ya kiwango kilichotajwa kisheria.
Watumishi hao wamepangwa kwa madaraja, ambapo daraja la kwanza litahusu watumishi wa ndani katika nyumba za waajiri wenye hadhi ya kibalozi na wa mashirika ya kimataifa.
Daraja hilo
la kwanza litahusu pia watumishi wa ndani katika nyumba za
wafanyabiashara mashuhuri, ambao kwa pamoja watalipwa kwa mwezi si chini
ya Sh 150,000, ambayo ni sawa na Sh 34,618 kwa wiki, Sh 5,769.70 kwa
siku na Sh 769.30 kwa saa.
Watumishi
katika nyumba za maofisa wenye nafasi za juu, watakuwa daraja la pili
na kulipwa si chini ya Sh 130,000 kwa mwezi, sawa na Sh 30,002.30 kwa
wiki, Sh 5,000.40 kwa siku au Sh 666.70 kwa saa.
Katika
daraja la tatu, kima cha chini kinahusu watumishi wa ndani ambao
wanafanyakazi kwa watu wengine mbali na maofisa wenye hadhi ya kibalozi,
wafanyabiashara mashuhuri na maofisa wa juu.
Watumishi
hao ni wanaofanya kazi na kuondoka jioni, ambao mshahara wao wa kima
cha chini kwa mwezi utakuwa si chini ya Sh 80,000, sawa na Sh 18,463 kwa
wiki na Sh 3,077.15 kwa siku au Sh 410 kwa saa.
Daraja la mwisho ni kwa wafanyakazi wengine wa ndani, ambao mshahara wao wa kima cha chini, utakuwa si chini ya Sh 40,000.
No comments:
Post a Comment