Maelfu
ya watoto wanaofanya kazi katika machimbo ya madini nchini Tanzania
wanakabiliwa na tishio kubwa la kupata magonjwa na hatimaye kufa.
Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human
Rights Watch, limefichua ushahidi zaidi kuhusu unyanyazaji wa watoto
nchini Tanzania, baadhi yao wenye umri wa miaka minane ambao wanafanya
kazi kwa zamu, katika migodi ya madini iliyoko chini ya ardhi, kwa saa
ishirini na nne.
Shirika hilo limesema watoto hao wanakabiliwa na
tishio la kuvuta hewa ya sumu inayotokana na uchimbaji wa madini ya
dhahabu na wakati mwingine kuuawa wakati migodi hiyo, inapoporomoka
nyingi zikiwa hazina leseni.
Tanzania ina sheria kali inayozuia watoto
kufanya kazi katika machimbo ya madini lakini shirika hilo limesema,
serikali ya rais Jakaya Kikwete ni sharti iimarishe juhudi zake za
kuhakikisha sheria hizo zimetekelezwa.
|
No comments:
Post a Comment