ZAIDI YA WATU 60 WAUWAWA KENYA KWENYE SHAMBULIZI LA KIGAIDI LA AL SHAABAAB.
Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama
Joseph Ole Lenku imesema kuwa zaidi watu 59 wamefariki katika shambulizi la
kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175
kujeruhiwa.
Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi
waliokua ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano wakiwa wamjificha katika sehemu
mbali mbali za jumba la Westgate.
Shirika la Red Cross awali katika
taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50
kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi
lililotokea Jumamosi mchana.
Milio ya risasi ilisikika katika jengo la
Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawashikilia watu ndani ya jengo ilo ambao sasa ni mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa.
Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na
ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo
huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali
wanazuiliwa ndani ya jengo hilo.
Watu 39 waliuwa baada ya wanamgambo hao
kushambulia jengo hilo nje katika eneo la kuegeshea magari na badae kuweza
kuingia ndani ya maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne
na kuwpaiga watu risasi hovyo.
Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki
ni jamaa zake. Miongoni mwa waliofariki pia ni mwanadiplomasia wa
Canada na raia wawili wa Ufaransa. Rais Kenyatta anasema kuwa wale
waliohusika lazima wakabiliwe na mkono wa sheria.
Jamaa na marafiki waliofika kujua hali ya jamaa
zao wamezuiwa kuingia ndani ya jengo hilo. Wengi wa waathiriwa
walifariki kutokana na majeraha yao.
Picha hizi hapo chini ni njinsi mambo yalivyokuwa yakiendelea
No comments:
Post a Comment