Hii uwenda ikawa ni fundisho kwa Viongozi wetu wa Afrika pia hasa Nchini kwetu Tanzania ambao wanapenda kujilimbikizia mali huku wakisahau wajibu wao wa kuwatumikia wananchi kama walivyohapa kwenye Katiba na wananchi watakapo kasilika na kuingia mtaani ndio mambo kama haya hutokea.Picha ya kwanza hapo juu ni Makazi binafsi ya aliekuwa Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych yalivyokutwa baada ya kuikimbia nchi hiyo Kodi za watu zimetumika kuyafanya kama hivyo yanavyoonekana.
Hili ni sinki la kunawia mikono tu lilivyonakishiwa na vito vya thamani huku akijua ni makosa kutumia kodi za wananchi vibaya uku maisha ya wananchi anaowaongoza ni Magumu.
Mwisho wa Siku Wananchi wanaamua kuandamana na kufanya uharibifu kama hivi kwenye Picha kwa uzembe tu wa Kiongozi waliomuamini na kumchangua mwisho wa siku anabadilika na kutowajali wananchi wake.
|
|
No comments:
Post a Comment