Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars,
Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni
siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo ulitangazwa jijini Dar es
Salaam na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele
ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha
Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia
kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa
kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa
kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi
amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha
kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5
mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa
Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
atalipa nusu ya gharama zilizotokana na shirikisho hilo kuvunja mkataba
wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen.
"Tulichokubaliana ni siri na kitabaki kuwa siri, TFF tutabeba, wapo
wadau waliojitokeza kutulipia nusu kwa sababu waliahidi kuwa huu ni
wakati wa mabadiliko," alisema Malinzi na baadaye kubadili kauli ya
wadau na kujitaja yeye kuwa ndiye atakayelipa gharama hizo.
Ingekuwa vizuri ukawaeleza maelfu ya watanzania wapenda soka ni wadau gani mtakao shilikiana nao ili umma wa Tanzania kuwajua na si vibaya kama wakapongezwa kwa ilo. Na wengine wameoji mamba haya kwenye Baadhi ya Mitandao ya Kijamii hapo chini..
Ukiwa kama Rais wa TFF, Je shirikisho lina mgogoro wa kifedha kiasi kwamba haliwezi kabisa kulipa fidia hiyo?
Je huoni kwamba unatujemgea wasiwasi kua unajenga mazingira ya kujilipa hapo baadaye, tena zaidi kwa njia zisizo halali?
Je
hii sio njia ya kuwa intimidate viongozi wengine ili waogope kuhoji
baadhi ya matumizi yako ya pesa kwa kuwa tu umeanza na visingizio vya
kutumia pesa zako Binafsi.
Je huoni kuwa hii ni
conflict of interest?? Kwa nini utumie Pesa yako tena bila kuutangazia
uma ni kiasi gani wakati shirikisho lina uwezo wa kulipa pia
kama
kweli una nia hiyo thabiti, kwa nini msiwatangazie wana michezo kiasi
halisi unachojitolea wewe mfukoni mwako... na kiasi anachodai Poulsen
|
No comments:
Post a Comment