Ripoti iliyosubiriwa kwa hamu kuhusu ufisadi nchini
Afrika Kusini, imemkosoa vikali Rais Jacob Zuma kwa kujinufaisha na pesa
zilizotumiwa kuikarabati nyumba yake binafasi katika mkoa wa Kwazulu
Natal.
Ukarabati huo uligharimu dola milioni 23.
Katika ripoti yake , mdhibiti wa
mali ya umma nchini humo,Thuli Madonsela, amesema kuwa Zuma alikiuka
sheria za maadili na kujifaidisha na pesa za Umma.
Inaarifiwa Zuma alisisitiza ukarabati huo, ufanywe.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilisema kuwa
hakudanganya wabunge kuhusu kashfa hiyo. Kadhalika wito umetolewa kuwa
Zuma arejeshe sehemu ya pesa hizo ambazo hazikutumika kwa ajili ya
usalama wake au vinginevyo.
Vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa
baadhi ya pesa za umma zilitumiwa katika kufadhili mahitaji ya kifahari
ya bwana Zuma kama bwawa la kuogelea na chumba cha sinema.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema kuwa ripoti
hiyo itaathiri pakubwa sifa ya Zuma na chama tawala ANC, huku
akijiandaa kwa uchaguzi mkuu katika kipindi cha wiki sita.
Zilivyokuwa kabla ya ukarabati huo kufanyika
|
No comments:
Post a Comment