Sunday, May 4, 2014

DIAMOND KAVUNJA REKODI YA TUZO ZA KILI MUSIC ACHUKUA TUZO 7

Hatimaye zile Tuzo za Muziki Tanzania Zinazojulikana kama Kili Music Award ndio zimemalizika na Mwanamziki Diamond Kuibuka na Tuzo saba katika Vipengele tofauti tofauti.

 


Monday, April 14, 2014

HATIMAYE HATI HALISI YA MUUNGANO ITAWASILISHWA BUNGENI SIKU MBILI ZIJAZO.

Mwenyekiti wa kamati namba Sita Mh.Stephen Wasira kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amethibisha rasmi leo ndani ya Bunge la Katiba na kwa wananchi wa Tanzania kuwa Hati alisi ya Muungano ilisainiwa na Marais wawili Mwl.Julius Nyerere na Mwezake Abed Karume miaka hamsini iliopita ipo na itwasilishwa rasmi katika Bunge la Katiba ndani ya siku mbili zijazo,namnukuu Wassira: Nalihakikishia Bunge kuwa Hati ya Muungano wa Tanzania ipo na itawasilishwa Bungeni siku mbili zijazo!

Kwa hatua hiyo ya kuitoa Hati halisi ya Muungano itakuwa imesaidia kupunguza maneno kutoka Baadhi ya wajumbe kuwa hati hiyo aipo na kama ipo basi si halisi bali itakuwa imechakachuliwa.

Wakati mijadala ya kamati ikiwa inaendelea kuliibuka swala la wajumbe kutaka wapatiwe hati ya muungano na hata ilipopatikana ilionekana kama baadhi ya saini zilizopo zimegushiwa.

 Leo aliekuwa Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya muungano mzee Pius Msekwa alipokuwa amazungumza kupitia kituo cha tv cha Taifa (TBC1) Amesema kuwa kuwa hakuwahi kuziona na wala hazikuwahi kuletwa bungeni badala yake, kile kilicholetwa bungeni ile tarehe 25/04/1964, ili kuridhia hati hizo, sio Hati Halisi za Muungano, bali ililetwa Sheria ya Muungano, ikiwa imeambatanishwa na "a schedule" ya Hati Hizo, iliyokuwa imepigwa chapa tuu, bila saini yoyote!.

 


Sunday, April 13, 2014

LIVEPOOL 3 MANCITY 2 .

Mpira umemalizika kati ya Liverpool na Manchester City na liverpool kuibuka na ushidi wa Mabao 3 kwa 2.Liverpool walikuwa mbele kwa mabao 2 mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika kwa magoli ya Halftime na Skirtel dakika ya 26.Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana na kupelekea Man City kurudisha magoli hayo yaliofungwa na Silva dakika ya 56 pamoja na Johnson aliejifunga kwenye Dakika ya 63 Goli la ushidi la liverpool limefungwa na beki wa Machester city na naodha wa Timu hiyo Vicent kwa matokeo hayo Liverpool imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu wingereza kwa point 77


GWIJI WA MZIKI WA DANSI MUHIDIN GURUMO ATUNAE TENA KATIKA DUNIA HII.

Mwanamziki na Gwiji wa mzuziki wa dansi nchini Tanzania mzee Muhidin malimu Gurumo alikuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo ngoma  amefariki majila ya mchana katika Hospitali moja alipokuwa akipatiwa matibabu.


Habari za hivi punde:Elkopta ya Polisi imeaguka Dar es salaam.

Habari za awali zinasema kwamba kulikuwa na baadhi ya viongozi waliokuwa katika ziara ya kukagua athali za mafuriko jijini Dar es salaam

Habari zinazoendelea kupatikana ni kwamba ilikuwa na Kamanda wa Polisi wa kanda maalum pamoja na Mkuu wa mkoa lakini wanaendelea vizuri habari zaidi zinafuata......... 

 Habari zaidi zinasema pia kulikuwa na makamu wa rais katika msafara huo



MANNY PACQUIAO AMSHIDA TIM BRADLEY

Pambano la ngumi kati ya Manny Pacquiao na Tim Bradley limemalizika mda mfupi uliopita kwa Manny kushinda kwa point kama ambavyo Bradley alivyoshinda kwenye pambano la kwanza kati yao ingawaje baadhi ya watu hawajalidhika na ushidi huo na kusema ni kama alioupata Tim katika pambano la kwanza wa utata utata.

 


Saturday, April 12, 2014

ARSENAL HATIMAYE WATINGA FAINALI YA KOMBE LA FA.

Hatimaye Timu ya Arsenal sasa imejiweka katika mazingila mzauri ya kuibuka na kikombe msimu huu baada ya kutiga Fainali ya chama cha mpira cha wingereza maarufu kama Kombe la FA baada ya kuifunga timu ya wigani kwa Penati 4 kwa 2 za Wigan baada ya kumaliza mchezo huo kwa kufungana magoli 1 kwa 1

  Kipa wa Arsenal akiokoa moja ya Penati