BAADA YA KUTAKA KUJIONGEZEA MISHAHARA WABUNGE KENYA WAFANANISHWA NA "NGURUWE"
Polisi nchini Kenya wamekabiliana na waandamanaji
waliozingira majengo ya bunge kulaani jaribio la wabunge kutaka
kujiongeza mishahara.
Polisi hao wametumia gesi ya kutoa machozi
pamoja na maji kuwatawanya waandamanaji hao ambao wengi wao ni wanachama
wa mashirika ya kijamii ambao wamesma katu hawaondoki katika majengo
hayo ya bunge hadi wabunge watakapopata ujumbe wao.
Pia inaarifiwa kuwa wanawataka
wabunge kutia saini na kuapa kuwa hawatatumia bunge kunyanyasa wananchi
maskini kwa kujiongeza mishahara kinyume na sheria.
Mashirika ya kijamii yaliandaa maandamano hayo
kuonyesha ghadhabu waliyonayo wakenya dhidi ya wabunge hao wanaotaka
kuongezwa miashara, miezi miwili tu baada ya kufanyiika uchaguzi mkuu wa
amani.
Aidha waandamanaji hao walipeleka Nguruwe kwenye
mlango mkuu wa kuingia katika bunge pamoja na damu kama ishara kuwa
wabunge ni watu walafi na wasiojali maslahi ya wakenya kwa kujitakia
makubwa.
Maandamano haya yanakuja siku moja baada ya tume
ya kitaifa ya mishahara ambayo wajibu wake ni kudhibiti mishahara ya
wafanyakazi wa umma kusema kuwa katu haitawaongeza mishahara wabunge.
Tume hiyo ilisema siku ya Jumatatu kuwa
haitaogopa vitisho vya wabunge kutaka kuivunjilia mbali tume hiyo ikiwa
hawatawaongeza mishahara wabunge kama kikwazo.
Wabunge hao walijaribu kwa kutumia vitisho kuilazimisha tume hiyo kuwoangeza mishahara lakini hawakufua dafu.
Ni baada ya mbunge mmoja kuwasilisha hoja bungeni kuwa ikiwa tume hiyo haitawaongeza mishahara watafanyya kila hali kuivunja.
Hata hivyo tume hiyo ni ya kikatiba.
Wabunge wa Kenya wanataka kulipwa mshahara wa
shilingi 850,000 wakati wakihudumu katika bunge la kumi ikipuuza
mshahara waliowekewa na tume ya mishahara ambao ni shilingi 532,000.
Wanasema pesa hizi ni kidogo sana.
No comments:
Post a Comment