Thursday, May 9, 2013

HUYU NDIE KOCHA MPYA WA MACHESTER UNITED.

Hatimaye sasa ni wazi kuwa Kocha mpya wa timu ya Machester united ni Divid Moyes baada ya kutangazwa rasmi mda mchache uliopita kwa masaa ya Afrika Mashariki na kati na ni baada ya kusaini mkataba wa Miaka 6 kuifundisha Machester united.

Kocha huyo mwenye Umri wa miaka 50 anachukua nafasi ya Sir Alex Ferguson kuanzia july 1.Moyes ambae alikuwa kocha wa vijana wa Goodison Park Everton toka mwaka 2002 alitangaza kuachia nafasi yake katika timu ya Everton mda mchache mara baada ya tamko la sir ALEX.

 "Wakati tunajadili mtu wa kunirithi wote tulikubaliana kuhusu David Moyes.
"David ni mtu makini mwenye miiko ya kazi. Nimekuwa nikipenda ufanyaji wa kazi yake kwa muda mrefu na niliwahi kumshawishi mwaka 1998 ajiunge nami kuwa msaidizi wangu hapa. Akiwa kijana mdogo na akiwa ndio anaanza maisha yake ya ukocha na tangu wakati huo amekuwa akifanya kazi nzuri na klabu ya Everton, Maneno ya kibabu Ferguson hayo.

HUYU NDO MRITHI WA SIR ALEX FERGUSON KUANZIA JULY 1.

No comments:

Post a Comment