Monday, June 10, 2013

HALI YA AFYA YAKE IKILIPOTIWA KUANZA KUIMALIKA MAOMBI YA KUMUOMBEA. YAENDELEA.

Rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini Mzee Nelson Madiba Mandela ameendelea kusalia Hospitalini  tangu alipolazwa  kutokana na matatizo ya mapafu yaliyoathiri mfumo wake wa upumuaji.

Maombi yanaendelea kufanyika katika makanisa na sehemu mbalimbali Duniani na kwa mtu mmoja mmoja  nchini Afrika kusini kumuombea afuweni Mzee Mandela anayeendelea kupokea matibabu hospitalini mjini Pretoria.

Taarifa kutoka ikulu inaeleza kwamba Bwana Mandela ambaye ana umri wa miaka 94 anapumua mwenyewe pasipo usaidizi wowote.

Anaumwa mno lakini hali yake inaimarika,Alisema msemaji wa Mzee Mandela.

Rais Jacob Zuma ameashiria kwamba atamtembelea Mandela punde tu madaktari watakapotoa ruhusa.

Hii ni mara ya tatu kwa Mzee Mandela kulazwa hospitalini katika muda wa mizezi sita iliyopita.

Msemaji wa chama tawala cha ANC,Keith Khoza amesema anamini Mzee Mandela atapona.

HILI NI GAZETI LA AFRIKA KUSINI LILIVYOANDIKA.
NASI KWA NIABA YA UONGOZI WA BLOG HII TUNAKUOMBEA AFYA NJEMA TUKIUNGANA NA WASOMAJI WETU PIA WANAOKUTAKIA AFYA NJEMA.

 

No comments:

Post a Comment