Mtangazaji mmoja wa tv nchini Tanzania alipost hii taarifa katika mtandao wake wa Instagram katika picha inayoonekana hapa
Basi katika kutafuta huku na kule ili kujua kwa undani zaidi nikakutana na hii pia si mbaya tukishilikiana wote kufahamishana maana inasikitisha kama ni kweli tazama picha hizi
hizi hapo juu ndo picha zake na ya katikati ni baada ya kukamatwa akiwa na Madawa hayo ya kulevya na inasemekana Msichana huyu makazi yake ni Ilala Dar es saalam inasadikiwa kuwa huwenda akanyongwa ijumaa huko misiri kama ni kweli narudia tena kama ni kweli.
*******************************
Ikiwa leo ndo ile siku ambayo inasemekana ndio siku ambayo Dada Mtanzania ananyongwa atimae Wizara ya Mambo ya nchi za nje na husiano wa kimataifa kupitia kwa Mkuu wake wa kitengo cha habari umetoa taarifa kama tulivyo ichukua kwa msaada wa Gazeti la Mwananchi kama muendelezo wa habari hii...
Akizungumza na Mwananchi jana Mkuu wa Kitengo cha
Habari cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mkubwa Ali,
alikiri kukamatwa kwa watu hao (majina yanahifadhiwa) ambao mmoja ni
mkazi wa Ilala na mwingine wa Magomeni jijini Dar es Salaam. “Taarifa
tulizonazo zilizo rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa sasa
ni kukamatwa kwa Watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha heroin
kuelekea Bara la Asia na walikamatwa nchini Misri wiki mbili
zilizopita.”
“Tumewasiliana na balozi wetu nchini Misri amesema
hana taarifa za kuhukumiwa kunyongwa kwa watuhumiwa hao, isipokuwa
wameshasomewa shtaka lao la awali. Wapo rumande kwa sasa kwani kesi hiyo
imetajwa mara moja tu. Balozi amekiri kushikiliwa kwa watuhumiwa hao
wakiwa na dawa zinazoaminiwa ni za kulevya,” alisema.
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa polisi na wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Video inayomwonyesha mmoja akikaguliwa na maofisa
wa polisi wa nchini Misri na kukutwa na dawa hizo, ilisambaa siku nne
zilizopita katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kwa mujibu wa sheria za Misri kama ilivyo kwa nchi
za Bara la Asia, mtu akikamatwa na dawa za kulevya hukumu yake ni
kunyongwa hadi kufa. Kutokana na sheria za nchi hiyo, tangu kukamatwa na
Watanzania habari zimeenea kuwa huenda wakanyongwa.
Habari za uhakika kutoka kwa ndugu wa karibu wa
mtuhumiwa huyo, zilidai kuwa walikuwa hawafahamu kuwa alikuwa
anajihusisha na dawa za kulevya.
“Huyu ni ndugu yangu kabisa lakini nilikuwa sijui kama anafanya mambo kama hayo’’ alisema.
kama atanyongwa ni pigo kubwa kwetu,” alisema mmoja wa ndugu wa Sharifa ambaye hakupenda kutaja jina lake.
Alisema miaka mitatu iliyopita ndugu yao wa kike
mwenye mtoto mmoja alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Nivea na
alikuwa hana tabia mbaya.
Jana Mwananchi lilifika katika Ubalozi wa Misri
nchini ili kufahamu kwa kina habari hizo, ambapo balozi wa nchi hiyo
hakuweza kuzungumzia lolote.
No comments:
Post a Comment