KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji
cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16)
anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa
ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo
anaonekana pichani.
Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika
mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine
wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana
huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya
Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi
miwili iliyopita.
Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto,
alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili
akamnunulie soda.Aliliambia Majira kuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta
bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata
mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata
ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga
kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo
wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza kusema kuwa ni
uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula
ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana
na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa
bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu
anayetafuna hindi la kuchoma.
“Mshtakiwa huyo alianza
kumtafuna jicho moja na kufuatia jicho la pili na kisha kumeza vipande vya
macho huku akiendelea kumshika kwa nguvu,” alisema DC Mwamotto wakati wa
mahojiano na Majira.
Baada ya kumaliza
kitendo hicho alisema kuwa mshtakiwa huyo alianza kumng’ata pua na kisha kumeza
na vipande.
Alisema kuwa wakati
anaendelea na kitendo hicho majeruhi huyo alikuwa akipiga kelele za kuomba
msaada, lakini mshtakiwa huyo alianza kumng’ata tena kipande cha mdomo wa chini
na kisha kusababisha meno kubaki nje.“Kutokana na kelele hizo wananchi waliamua
kusogea karibu, lakini walikuta tayari, Susuluka amejeruhiwa vibaya usoni huku
damu zikimtoka kwa wingi,” alisema.
Mwamotto alisema kuwa
kutokana na hali hiyo wananchi walimvamia na kumpiga na kumpeleka katika Kituo
cha Polisi cha Kibondo na majeruhi walimkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya
Kibondo.
Majira iliendelea na mahojiano hayo ambapo, mshtakiwa
huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya na kufunguliwa mashtaka ya kudhulu
mwili.“Hivi sasa mshtakiwa yupo katika Gereza la Nyamisivi Kibondo, lakini cha
kusikitisha tena akiwa huko alimng’ata na kula vipande vya nyama vya mguu
mshtakiwa mwenzake,” alisema.
Alisema kuwa mshtakiwa
mwenzake alimjeruhi vibaya na kupelekwa hospitalini hali iliyosababisha
mshtakiwa huyo kutengwa na washtakiwa wenzake.“Mimi nimelazimika kwenda hadi
gerezani na kufanya mahojiano na mshtakiwa huyu, kwani hili tukio linasikitisha
sana lakini cha ajabu alitaka kufahamu je ameshtakiwa kwa makosa gani ya kuua
mbwa au kumng’ata mtu,” alisema.
Alisema kuwa pia
amelazimika kwenda kumjulia hali majeruhi huyo ambapo madaktari katika
hospitali hiyo walishindwa kumtibia.“Nimeomba msaada kutoka Wizara ya Afya ili
mgonjwa
huyu akatibiwe India na
tayari maandalizi yameanza kufanyika kwa kushirikiana na Hospitali ya Kibondo,”
alisema.
Mwamotto alisema kuwa
mgonjwa huyo hana pua, macho yamefumba, mdomo kwa kujeruhiwa vibaya usoni hali
ambayo anahitaji matibabu zaidi.Amewaomba Watanzania kumsaidia kijana huyo ili
aweze kwenda kutibiwa haraka nje pamoja na kupata msaada mbalimbali kwa
kuwasiliana na mganga mkuu wa hospitali ya Kibondo ama kuwasiliana na Mhariri
mtendaji wa gazeti la Majira
Habari hii kwa hisani ya gazeti la majira la Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment