Hatimaye hayawi hayawi sasa yamekuwa Mara baada ya usiku wa manane kwa saa za wingereza kuzaliwa Mtoto ambae anakuwa ni wa Tatu katika Urithi wa Ufalme wa Wingereza na pia Anakuwa ni Kitukuu kwa Malikia Elizaberh wa II wa Wingereza na pia anakuwa Mtoto wa kwanza wa kiume katika Familia ya Prince William na Anakuwa ni Mjukuu wa Prince Charles.Mtoto huyo wa kiume alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 8,na mtoto huyo ambae ni wa tatu katika urithi wa kiti cha ufalume kwa mujibu wa utaratibu siku moja atakuja kuwa Mkuu wa majeshi na pia mkuu wa nchi 54 za jumuhiya ya Commonwealth.
Mke wa mjukuu wa mfalme wa Uingereza, Prince William
amejifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya St.Mary's, Paddington
Mashariki mwa mji wa London.
Katika taarifa ya Kasri la kifalme la
Kensington, Duchess wa Cambridge amepata mtoto wake wa kwanza majira ya
saa kumi na dakika ishirini na nne za jioni kwa saa Uingereza,akiwa
amezaliwa na kilo 3.62874.Kasri la Kifalme limesema, mama na mwanawe wanaendelea vyema na watasalia hospitalini usiku huu.
Baba wa Mtoto, Prince William alishuhudia wakati mtoto akizaliwa.
Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto limetolewa na kuonyeshwa mbele ya lango kuu la Kasri kuu la kifalme la Uingereza la Buckingham kama utamaduni na mila za Uingereza zilivyo.
Taarifa rasmi iliyosainiwa na jopo la madaktari bingwa kuthibitisha kujifungua kwa Duchess wa Cambridge ilipelekwa kwenye kasri la kifalme chini ya ulinzi wa polisi.
Malkia wa Uingereza,Duke wa Edinburgh,Prince wa Wales, Duchess wa Cornwall na Prince Harry pamoja na wanandugu wa familia zote wametaarifiwa juu ya kujifungua salama kwa Kate na wote wamepokea vizuri habari hii, Imesema taarifa hiyo ya Kasri la kifalme
Hichi ni cheti cha usibitisho kuwa Mtoto amedhaliwa |
Umati wa watu waliofulika nje ya jengo mara baada ya taarifa ya Kate william kujifungua salama kutolewa. |
Wazazi wa Mtoto huyo. |
Huu ni mnara wa London BT Tower ukitoa ujumbe wa mtoto kuwa ni Mvulana. |
Watu walikesha wakisubili na wengine walipitiwa na usingizi kwa mda |
No comments:
Post a Comment