Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini Tanzania imesema karibu nusu ya watu waliojitokeza kupima vinasaba maalufu kama (DNA) ili kujua kama watoto ni wa kwao ama sio vipimo hivyo vimeonyesha si Wazazi halisi wa watoto hao.Takwimu hizo ni kwa muda wa kipindi cha kuanzia miaka mitatu kuanzia Mwaka 2010 ikionyesha kuwa asilimia 48.32 ya Wazazi wanalea watoto wasio wao wakati Asilimia 51.68 ndio Wazazi halali.Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu wa kitengo cha Makosa ya Jinai,Vinasaba na Baiolojia wa Ofisi ya Mkemia Mkuu Gloria Machuve. Swali la kujiuliza kwa takwimu hizi Swala la Uaminifu ni tatizo kwa wote wawili wewe unasemaje juu ya ili swala Tuandikie bpromas@outlook.com
|
No comments:
Post a Comment