HIVI NDIVYO MASHUJAA WETU WALIVYOPOKELEWA MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA AMINA.
Miili ya
wanajeshi saba mashujaa wa Tanzania waliofariki wakiwa kazini
wakitekeleza ulinzi wa amani wa kimataifa katika mkoa wa Darfur nchini
Sudan, iliwasili kwa ndege maalumu ya Umoja wa Mataifa.
Kaimu Mkurugenzi wa habari wa JWTZ, Meja Joseph Masanja amesema miili mara baada ya zoezi ya kupokelewa imehifadhiwa katika hospitali ya jeshi ya
Lugalo hadi Julai 22 ambapo itaagwa rasmi.
Miili iliyowasili ni ya Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula,
Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Pte. Rodney Ndunguru, Pte.
Peter Werema na Pte. Fortunatus Msofe.
Shughuli za kuagwa miili ya wanajeshi hao zitafanyika katika viwanja vya
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa vilivyoko Upanga jijini Dar
es salaam.
No comments:
Post a Comment