Kwa mujibu wa
ripoti ya Shirika la Transparency International, Tanzania imeshika
nafasi ya kumi na mbili kwa ufisadi ikiwa ni miongoni mwa nchi 107
ambako utafiti huo ulifanywa ukihusisha wananchi 1001 wa Tanzania.
Ripoti hiyo
ilibaini kwamba Watanzania karibia sita kati ya 10 waliohojiwa walisema
wamewahi kutoa hongo maishani mwao ili waweze kupata huduma moja hadi
nane kati ya zilizochunguzwa.
Kulingana na
utafiti huo, wananchi 87% walisema maofisa wa polisi ndio wanaongoza kwa
ruswa wakifuatiwa na mahakama (86%) hospitalini (79%), wafanyakazi wa
serikali (75%) sekta ya elimu (74%) na vyama vya siasa (68%)
Watanzania 23% walisema taasisi za kidini zinajihusisha na ruswa wakati Jeshi (38%) na vyombo vya habari (41%).
Asilimia 3 ya Wakenya na Watanzania waliohojiwa walisema rushwa
imepungua tofauti na asilimia 56 ya Warwanda huku asilimia 1 ya Waganda
na Warundi wakidai vivyo hivyo.
Nchi fisadi zaidi
duniani ni Sierra Leone ambako asilimia 84 ya watu waliohojiwa
walikubali kwamba wametoa hongo. Sierra Leone inafuatwa na Liberia
(asilimia 75) na Yemen (asilimia 74).
Nchi ambazo
zilipatikana kuwa na ufisadi finyu ni Finland, Japan, Australia,
Denmark, Uhispania, Canada, Ureno, Uruguay, Norway, New Zealand, Korea
Kusini na Malaysia ambako watu zaidi ya 95 kati ya 100 waliohojiwa
walisema hawajaona ufisadi wowote nchini mwao.
Katika eneo la
Afrika Mashariki, Kenya ndiyo nchi fisadi zaidi ikifuatwa na Uganda
(asilimia 61) na Tanzania (asilimia 56). Kulingana na utafiti huo ambao
watu 114,000 walihojiwa, Rwanda ilipatikana kuwa na ufisadi mdogo zaidi
katika eneo la Afrika Mashariki. Raia 13 pekee kati ya 100 wa nchi hiyo
walikubali mwamba wametoa hongo. Ufisadi ulipatikana kukithiri zaidi
barani Afrika. Baadhi ya nchi fisadi zaidi Afrika ni Zimbabwe, Msumbiji,
Libya na Cameroon (zote zikiwa na asilimia 62) na Nigeria (asilimia
44).
Njia iliyotumia ni kwa kupata maoni kwa njia ya maswali ambapo wananchi
zaidi ya 1000 kwa kila nchi 107 walihojiwa na kujibu maswali uso kwa uso
na kwa njia ya elecroniki kati ya Sept 2012 mpaka March 2013.
Kwa nchi za afrika ya mashariki, wananchi walihojiwa kwa njia ya uso kwa
uso na makampuni ya TI kenya, TI Rwanda na Infinite insight katika
maeneo ya mjini na vijijini.
|
No comments:
Post a Comment