Thursday, July 11, 2013

CHADEMA KUANZISHA MAFUNZO KWA VIJANA ILI KUJILINDA HII NDO KAULI YA AMIRIJESHI MKUU.

  Baada ya Chadema kusema kwamba wataanzisha mafunzo kwa vijana wao kwa ajili ya kuwalinda ikidai kuwa dola imekuwa haisikilizi madai yao.Hatimaye Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ambae pia ndio amirijeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Nchini Tanzania amesema kuwa

“Chama cha siasa kuanzisha kikundi cha wanamgambo kwa ajili ya kupiga watu ni kiashiria kwamba chama hicho hakitaki amani bali kinaridhishwa na vurugu,” alisema na kuongeza kuwa wanaopenda amani humaliza tofauti zao kwa kuzungumza".

“Tusiiache nchi yetu ije kulindwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa, tusije kufikia huko, tujitahidi kuondoa tofauti zetu kwa njia ya mazungumzo,” aliyasema hayo wakati akifunga kongamano la kujadili Amani lililoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).Ambapo Chadema ilisusia kongamano hilo ikisema kuwa amani haitafutwi kwa kufanya makongamano kama ilivyofanya TCD.

Rais pia akaongeza kwa kusema wanaosusa kongamano hilo wangeweza kufika wangeweza kutoa madukuduku yao kwa sababu viongozi wa Serikali na polisi walikuwapo lakini bado hawataki.

“Sasa hawa kweli wanapenda amani yetu wakati hawapendi kuja tuzungumze, wanataka watu wauane ama wapigane,” alisema kwa mshangao huku akiendelea kusema

 Serikali na viongozi wake hawapendi vurugu na kwamba chama hicho kinafanya vurugu hizo ili kuwatoa katika ajenda za kuwaletea maendeleo Watanzania.

 


No comments:

Post a Comment