Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania Samuel Sitta ambae kwa sasa ni Waziri wa Afrika mashariki amenukuliwa akisema“Ninakerwa sana na mfumo wa Viti Maalumu, kwanza sioni umuhimu
wa mfumo huu kuendelea kuwepo katika Katiba Mpya. Hawana umuhimu
wowote.”
Katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika Uwanja
wa Shule ya Msingi Nyamikoma, Kata ya Busega Mkoa wa Simiyu Julai 29,
mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kampeni za kuimarisha uhai wa chama, Sitta
aliwajia juu bila ya kuwataja baadhi ya wabunge wa CCM.
“Wanakwenda bungeni hawachangii, hawana hata hoja
za kuchachafya upinzani, hawachangii, hawa ni mzigo,” alisema Sitta na
kuongeza: “Wapo baadhi ya wabunge, hawajawahi hata siku moja kwenda
kwenye majimbo yao kuwatembelea wananchi waliowachagua... Inawezekana
hata wapiga kura wakawa wamewasahau. Hawa hawafai hata kuchaguliwa
wakiomba tena kura.”
“Rais Jakaya Kikwete amejitahidi sana kuleta
mabadiliko, ameleta mafanikio ya uchumi na mambo mengi. Inatakiwa
wabunge waende wakawaeleze wananchi maendeleo haya, inawezekana
hawayajui lakini watu hawaendi jimboni, wananchi watayafahamu vipi haya
maendeleo?”
Juzi, akizungumzia wabunge wa Viti Maalumu, Sitta
alisema... “Wengi wao hawachangii chochote na mbaya zaidi hakuna wa
kuwahoji chochote kama wabunge wanavyorudi jimboni.
“Ikifika wakati wa posho wapo. Sisemi kama naumia
wao kuchukua posho.... hawa wanachukua posho wanawajibika kwa nani? Nani
anahoji utendaji wao na zaidi itakapokuja Katiba Mpya ya kuwawajibisha
wabunge wazembe, hawa watawajibishwa wapi?”
“Rasimu ya Katiba Mpya isiwaruhusu hawa... hawa
nao ni mzigo mwingine. Wakifika bungeni hawachangii chochote, hawawezi
kuwajibishwa na yeyote kwa mfumo uliopo na pia hawawajibiki popote, sasa
huu si mzigo?”Ikumbukwe pia mke wake ni Mbunge wa viti maalum.
|
No comments:
Post a Comment