Picha hapo juu inamuonyesha mwanamke ambae anahofia
maisha yake baada ya kutambuliwa visivyo kwenye mitandao ya internet
kwamba yeye alikuwa shahidi katika kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya
William Ruto katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.
Mwanamke huyo anasema aliathirika na ghasia za
baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2008 lakini yeye si shahidi katika
makama ya ICC kama ilivyolipotiwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mama huyo Rahab Muthoni Kagiri
,mwenye umri wa miaka 27 kutoka eneo la Burnt Forest , huko Rift valley
anasema yeye sii shahidi katika kesi hiyo inayomkabili Naibu Rais wa
Kenya William Ruto pamoja na mtangazaji Joshua arap Sang.
Akionekana mwenye wasiwasi Bi Rahab asema sie
yeye aliyesimama kizimbani kama shahidi wa kwanza katika kesi hiyo
kinyume na inavyodaiwa na mitandao ya kijamii nchini Kenya.
Mama huyo anadia kuwa picha hiyo alipigwa na
rafiki yake kwa lengo la kuiweka katika mtandao wake wa Facebook majira
ya saa tano siku ya jumanne.
Lakini alishangaa saa mbili baadaye alianza
kupigiwa simu na jamaa , ndugu na marafiki wakisema wameona picha yake
katika mtandao ukisema yeye ndie shahidi aliyetoa ushahidi dhidi ya
naibu Rais Wiliam Ruto.
Bi Rahab anasema japo yeye pia ni muathiriwa wa
machafuko yaliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo watu zaidi
ya 1,00 waliuwawa lakini hajajitolea kutoa ushaidi katika mahakam hiyo
ya ICC.
Na kutokana na madai ya ufichuzi wa mashahidi
nchini Kenya , hii leo Mahakama ya ICC iliamuru shahidi wa kwanza ambaye
alianza kutoa ushaidi wake siku ya jumatatu atoe ushahidi wake
faraghani.
Hii nikutokana na kudaiwa kuwa na hofu nyingi
Hii hapo juu ndio Picha iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikisema huyo mwanamama ndio alikuwa shahidi wa kwanza kutoa ushaidi katika kesi hiyo na kupewa namba 536 na chini ni Mwanzo wa taarifa hizo zilipoanzia na kuanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
|
No comments:
Post a Comment