TAJI LA MUSLIM WORLD BEAUTY PAGEANT LIMECHUKULIWA NA....


Mwanadada wa Nigeria ndiye mshindi wa shindano la urembo kwa wasichana wa kiisilamu mjini Jakarta Indonesia.
Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alishinda shindano
la kimataifa la wasichana wa kiisilamu kwa jina Muslimah mwaka 2013 siku
ya Jumatano.
Washindani 20 walishiriki mashindano
hayo kuonyesha mitindo ya kiisilamu pamoja na maadili ya kiisilamu
wakati wa mashindano hayo.
Mashindano yalifanyika kabla ya shindano kubwa
zaidi la mwanamke mrembo zaidi duniani, ambalo limeghadhabisha makundi
ya watu wenye msimamo mkali nchini Indonesaia kwa kutaka kuandaliwa
huko.
Waliofuzu kwa fainali ya mashindano hayo, walichaguliwa kutoka miongoni mwa watu 500 waliochaguliwa kwa kutumia njia ya mtandao.
Moja ya vikwazo vya kuruhusiwa kushirki kwenye
mashindano ilikuwa kusimulia kisa chako na ambavyo ulianza kuvalia Hijab
au mtandio, ambacho kilikuwa kikwazo kwa wote waliotaka kushiriki.
Washiriki walitoka Bangladesh, Iran, Malaysia, Nigeria na Brunei.
Kabla ya fainali, washindani walihitajika kuamuka kwa sala ya asubuhi na kuswali pamoja huku wakijifunza kusoma Koran.
Bi Ajibola, mwenye umri wa miaka 21, alilia na
kusoma aya kutoka kwa Korani, jina lake lilipotajwa. Alituzwa dola
2,200, pamoja na ziara ya mji mtukufu wa Mecca na nchini India.
Kabla ya kushinda alisema kuwa nia yake ya
kushiriki mashindano hayo ilikuwa tu kuonyesha dunia nzima kuwa dini ya
kiisilamu ni nzuri sana.
Eka Shanti, aliyefutwa kazi kwenye televisheni
kwa kukataa kuvua mtandio wake, ndiye alianzisha shindano hilo miaka
mitatu iliyopita.
Aliambia shirika la habari la Agence
France-Presse kuwa walifanya shindano hili siku chache kabla ya shindano
la kimataifa la mwanamke mrembo zaidi duniani kuonyesha wasichana kuwa
kuna njia zengine tofauti ambazo unaweza kuwa mrembo.
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waisilamu duniani.
No comments:
Post a Comment