CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
tukio la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondolewa bungeni mjini Dodoma
kwa agizo la Naibu Spika, Bw. Job Ndugai, lilipangwa na Serikali ili
kuhakikisha Muswada wa sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba mwaka
2013, unapitishwa bungeni ili kulinda masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA, Bw. John Mnyika, ambaye
pia ni Mbunge wa Ubungo,Alisema Serikali ilipanga kupitisha muswada huo bungeni
ndio maana hata Bw. Mbowe kama Kiongozi wa Upinzani bungeni, aliposimama kutaka
kuzungumza, hakupewa nafasi hiyo badala yake alitakiwa akae na alipokataa Bw.
Ndugai aliagiza atolewa nje jambo ambalo hawakuliunga mkono.
Aliongeza kuwa, Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha
wabunge wa CCM wanakuwa wengi katika Bunge la Katiba ili kupitisha mambo
wanayoyataka."Kilichopitishwa bungeni na wabunge wa CCM ni kibaya kuliko
ilivyokuwa awali...wameharibu zaidi, CHADEMA imepinga kwa masilahi ya makundi
mengine ya kijamii ili yaweze kupata uwakilishi katika bunge hilo,"
alisema.
Bw. Mnyika alisema CHADEMA walipendekeza Bunge la Katiba lipunguze
uwakilishi wa chama kimoja ambapo katika kipengele cha wajumbe 166 wanaoteuliwa
na rais, iongozwe na kufikia wajumbe 359 lakini Serikali imekataa."Lengo
letu ni kutoa nafasi kwa makundi mengine ya kijamii kama wakulima, wafanyabiashara,
wafanyakazi na taasisi nyinginezo kutoa wawakilishi wao kwenye bunge
hili," alisema.
Alisema
upande wa Zanzibar, hakukuwa na wawakilishi waliotoa maoni yao juu ya nafasi ya
Zanzibar katika bunge hilo na kilichosemwa na Serikali ni uongo."Serikali
baada ya kushindwa kuchakachua Mabaraza ya Katiba, sasa imeona njia pekee ya
kufanya hivyo ni kuhakikisha kwenye Bunge la Katiba wabunge wa CCM wanakuwa
wengi," alisema.
Akizungumzia
uamuzi wa Bw. Ndugai kumtoa nje Bw. Mbowe, alisema Naibu Spika amevunja kanuni
ya 76 ya Bunge kwani hana nguvu ya kuita askari ambapo kwa mujibu wa kanuni ya
20, alitakiwa kuhairisha shughuli za Bunge."Ndugai amefanya kosa la
kuwaingiza watu wasiohusika bungeni na kuruhusu vitendo vya uhalifu vitokee ili
kupitisha muswada walioutaka na kulinda masilahi ya chama kimoja.
"Sekretarieti
ya CHADEMA itakutana ili kujadili kwa
undani suala hili na kulishughulikia, pia tutatumia nguvu ya umma (wananchi)
kuhakikisha katiba haivurugwi, tutakutana na vyama vingine vya upinzani,"
alisema.Alisema chama hicho hakioni sababu ya kuharakisha katiba badala yake
kama wanataka katiba hiyo itumike katika Uchaguzi Mkuu 2015 ni vyema
ikaandaliwa ya mpito.
Aliongeza
kuwa, katika Bunge lijalo Sheria ya Kura za Maoniambayo itajadiliwa ni ya
hatari zaidi kuliko Bunge la Katiba na isipofanyiwa marekebisho, itazusha
mgogoro mkubwa zaidi.
Maswali ya kujiuliza hapa kama Watanzania je?ni kweli Naibu spika alitumwa? na kama alitumwa ni kwa faida ya nani na kwa ajili ya nani?je amesahau kiapo alichoapa Bungeni?Kama majibu haya yasipopata majibu basi kunahaja kubwa katiba yetu Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote kile cha siasa bali waombe kulingana na sifa zao na badae chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kupitia maombi hayo kiyapitie kwa uwazi kabisa na wananchi wafahamu kabla ya kupitishwa na Bunge.
|
No comments:
Post a Comment