Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe (Mbunge)akiendelea kusisitiza kuwa hesabu za Chadema ni miongoni mwa Hesabu ambazo
hazijakaguliwa, chama hicho kimeishutumu kamati hiyo kwa kuagiza
kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa na kusema hatua hiyo ni ubabe.
Wakati Chadema wakitoa kauli hiyo, Zitto
alisema vyama vya siasa tisa vikiwamo Chadema, CCM na CUF vinatakiwa
kufika mbele ya PAC Oktoba 25 mwaka huu, kwa ajili ya kujieleza na
kwamba chama kitakachokaidi, sheria za Bunge zinaeleza wazi, kwamba
wahusika wanaweza kufungwa jela siku saba.
Chadema kilisema kuwa PAC kabla ya kuchukua hatua,
ilipaswa kuwapa nafasi ya kuwasikiliza viongozi wa vyama husika,
kumhoji Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Msajili
wa vyama vya Siasa ambao wameshindwa kutimiza wajibu wa kukagua hesabu
hizo kwa miaka minne.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony
Komu alisema jana kuwa, uamuzi wa PAC utaviathiri vyama kwani bajeti
zake zimezingatia kuwapo kwa ruzuku.
“Kuna vyama ambavyo vinategemea ruzuku kulipa
mishahara ya wafanyakazi wake, Chadema ingawa tuna vyanzo vingine vya
mapato, tunaitegemea kukamilisha bajeti yetu kwa fedha za ruzuku ambazo
zinatusaidia kwa asilimia 45. Ni tabia mbaya kuchukua uamuzi kwa kibabe
na kuhukumu kabla ya kutusikiliza siyo haki hata kidogo,” alisema Komu.
Alitetea chama chake kwamba kimekuwa na utaratibu
wa kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa ambapo alitoa ushahidi wa barua ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ya April 16, 2012 ikithibitisha kwamba hesabu
zao zipo sawa baada ya kuziwasilisha katika ofisi hiyo.
“Chadema tunataka ukaguzi wa hesabu usijikite
katika fedha za ruzuku pekee bali katika vyanzo vyote vya mapato ya
vyama, tatizo CAG alitueleza kwamba anakabiliwa na upungufu wa
rasilimali watu kwa hiyo PAC walipaswa kuliangalia tatizo hilo na
kutafuta ufumbuzi,” alisema Komu.
Zitto alikaririwa na vyombo vya habari
akieleza kuwa Serikali ilitoa kiasi cha Sh67.7 bilioni kama ruzuku kwa
vyama tisa vya siasa tangu mwaka 2009, lakini vyama hivyo havijawahi
kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu zake kwa msajili kama sheria
inavyoagiza.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema),
aliamuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kusimamisha utoaji
wa ruzuku hadi hapo vitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi na makatibu wake
wakuu kuhojiwa.
Vyama vya Siasa kuanzia mwaka
2009/2010 ambavyo vinapokea ruzuku na kiasi kikiwa kwenye mabano ni CCM (50.97bn/-), Chadema (9.2bn/-), NCCR-Mageuzi (677m/-),
CUF (6.3bn/-) and TLP (217M/-).
Others are DP (3.3m/-), APPT–Maendeleo (11m/-), UDP (333m/-) and CHAUSTA (2.4m/-).
|
No comments:
Post a Comment