Kampuni kubwa ya Tumbako nchini Korea Kusini ,
imeahidi kubadilisha tangazo lake la kibiashara ambalo limekosolewa kwa
kuonekana kuwa la kibaguzi.
Mabango yenye tangazo hilo la aina mpya ya
sigara ya kiafrika, yalikuwa na picha za Tumbili waliovalia kama
waandishi wa habari wakitangaza kuwa ''Afrika inakuja!''
Sigara hizo ni bidhaa mpya ya kampuni ya 'This Africa line'.
Aidha kampuni hiyo inasema kuwa sigara hizo zimetengezwa kwa Tumbako ya kiafrika na ambayo imekaushwa kwa njia za kitamaduni.
Paketi za Sigara zina picha zinazoonyesha Tumbili wakichoma tumbako hiyo.
Kejeli kwa Afrika
"tumeudhiwa sana na picha hii ya kejeli
iliyotumiwa na kampuni hiyo ikionyesha Tumbili na kuwahusisha na
Afrika,'' ilisema taarifa ya baraza la kudhibiti biashara ya
Tumbako Afrika kuwa sharti tangazo hilo liondolewe haraka
iwezekanavyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ''kukejeli Afrika
ili kuongeza mauzo ya bidhaa ambazo husababisha vifo na maradhi sio jambo
linalokubalika.''
Tangazo hilo la biashara limewekwa katika maeneo ya maduka kote nchini humo.
Hata hivyo msemaji wa kampuni hiyo ameelezea kuwa tangazo hilo litaondolewa madukani mwezi ujao.
Amesema kuwa kampuni imejutia utata
uliosababishwa na tangazo hilo na kusema kuwa kampuni hiyo ingependa
kuondoa wasiwasi wowowte ulioibuka kutokana na tangazo hilo kuhusu
ubaguzi wa rangi
Alisema hawakuwa na nia yoyote ya kuwakejeli
waafrika na kuwa walichagua kutumia tumbili kwa sababu ni wanyama wazuri
wanaowakumbusha watu kuhusu Afrika.
Kampuni hiyo inasema kuwa kwa sababu bidhaa hii
ina majani ya tumbako kutoka Afrika , nia ya kampuni ilikuwa tu
kufananisha bidhaa hiyo na Afrika.
|
No comments:
Post a Comment