Wednesday, October 23, 2013

TORRES APIGA 2 CHELSEA IKIIFUNGA SCHALKE 3-0,ARSENAL YAFUNGWA.

Mchezo wa Klabu Bingwa ulaya kati ya Chelsea na Schalke ya Ujerumani uliochezwa nchini ujerumani ulimalizika kwa Timu hiyo ya London C helsea kuibuka na ushindi wa Magoli 3 kwa 0 magali mawili ya Fernando Torres na lingine la Eden Hazard na kuifanya Timu Hiyo inayofundishwa na kocha Jose Mourinho kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata.

 Katika mchezo uliopigwa nchini Wingereza kati ya Arsenal na Timu ya Borussia Dortmund ulimalizika kwa Arsenal kukubali kichapo cha magoli mawili kwa moja kutoka kwa vijana hao wa nchini Ujerumani Goli hilo moja la Arsenal lilifungwa na Giroud kwenye dakika ya 41 ya mchezo huku yale ya Dortmund yakiwekwa nyavuni na Mkhitaryan dakika ya 16 na lingine la R. Lewandowski dakika ya 82 na kuwaacha vijana wa Arsene Wenger waliokatika kiwango cha juu kabisa kwenye ligi kuu ya wingereza wasiamini kilichowatokea.

 


No comments:

Post a Comment