Mbunge wa Musoma mjini kupitia chama cha Chadema ambae pia ni Waziri kivuli wa mambo ya Ndani Mh,Vicent Nyerere amedai kuwa Polisi wa Tanzania wanahari ngumu sana ya maisha na kufanya utendaji kazi wao kuwa mgumu sana ile hali wanamajukumu mazito ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
Waziri huyu Kivuli aliyasema hayo alipokua akizungumza maswala mbalimbali ikiwemo Operation tokomeza ujagili katika kituo kimoja cha television katika kipindi kinachorushwa kila siku ya jumatatu mara baada ya Taarifa ya habari.
Waziri kivuli wa mambo ya ndani,mh.Vicent Nyerere ameenda mbali kwa kusema
kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili polisi wetu leo hii ukamtumia
polisi ujumbe wa "tafadhali nipigie",yeye atakujibu kwa ujumbe wa
"tafadhali niongezee salio"!
Mh.Nyerere anasema inafikia hatua polisi anamsimamisha mwendesha
baiskeli na kumuhoji kwanini baiskeki yake haina madigadi,akaongeza kuwa katika kutafuta hela polisi wanamsimamisha mtu mwenye gari la
kubeba abiria wanne kwa mfano na kumuhoji ni kwanini yuko peke yake!Hizo
zote amedai ni mbinu za polisu kubambikizia watu(madereva) makosa ili
wapate fedha.
Mh.Nyerere ameenda mbali kwa kusema RPC anawapa kazi vijana wake za
kulisha familia.Yaani anawapangia wewe utalisha familia yangu akimanisha
askari hao watafute fedha wakiwa kazini na kumpelekea yeye(RPC),waziri huyo kivuli amezidi kusema kuwa hata hata viatu vya Polisi siku hizi havifanani kwani wanatafuta mtumbani.Yaani kila polisi anajitafutia sare za viatu vyake.
Kuhusu kumiliki siraha kiolela Waziri huyo kivuli alisema endapo angekuwa Waziri kamili angelishauli Baraza la mawaziri pamoja na rais kufuta vibali vyote vya kumiliki siraha na watu kuanza kuomba upya na kuweka utaratibu wa kuhakiki matumizi ya siraha hiyo matumizi yake,akatolea mfano katika jimbo lake kuna watu walinyimwa vibali vya kumiliki siraha za moto lakini wakatoka Musoma mjini wakaenda Shinyanga na Kigoma wakakubaliwa na kupewa kibali cha umiliki wa siraha,na alikubali kuwa siku hizi kuna madalali wa siraha.
Kuhusu hali za Wafungwa Magerezani amesema hali ni mbaya sana na yanaitaji mabolesho ya hali ya juu sana akatoa mfano kwamba wastani wa chakula kwa siku kwa mfungwa mmoja ni shilingi 500 ambapo hata maji huwenda usipate kwa pesa hiyo na akapendekeza kuwepo na utaratibu wa wale wafungwa wenye ujuzi mbalimbali kupelekwa katika sehemu za kijamii kuutumia ujuzi wao kwa kufanya kazi na sio kuishia kufagia na kukata Majani kwenye Nyumba za wakuu wa wilaya na wakuu wa Mikoa,Wakurugezi wa manispaa watumike kuwapangia wafungwa hawa kazi za kufanya kwani wao ndo wanamaeneo makubwa ya kuweza kujua ni kazi gani kuligana na utaaramu wa mfungwa husika.
|
No comments:
Post a Comment