Hayati Nelson Mandela, aliachia familia yake mali yake yenye thamani ya dola milioni 4.1.
Sehemu ya mali hiyo pia itatolewa kwa chama tawala ANC, wafanyakazi wake wa zamani na shule kadhaa ambako alisomea.
Hayo ndio yalikuwa mapenzi ya Mandela ambayo yalikuwa kwenye wasia wake uliosomwa hadharani kwa familia nzima.
Afisaa Dikgang Moseneke aliyekabidhiwa jukumu la
kusoma wasia huo wenye kurasa 40 na kuhakikisha unatekelezwa ,alisema
hapajakuwa na pingamizi zozote kuhusu yaliyomo kutoka kwa familia ya
Mandela.
Wafanyakazi wa karibu wa Mandela watapata randi
50,000 kila mmoja. Shule ambazo Mandela alisomea zitapata randi laki
moja kila shule.
Hayati Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95.
Familia ya Mandela tangu hapo imekuwa ikizozana
kuhusu urithi wa hayati Mandela na kuna hofu kuwa huenda wasia huu
ukasababisha mgogoro mwingine kuhusu mali hiyo.
Mali ya hayati Mandela inajumuisha nyumba na
hakimiliki za vitabu ikiwemo kimoja kuhusu maisha yake kwa jina ''Long
walk to freedom''
|
No comments:
Post a Comment