Mlemavu mmoja kutoka Denmark Dennis Aabo amekuwa
binadamu wa kwanza kupewa mkono wa kieletroniki wenye hisia kama ule wa
binadamu.
Katika
tukio linalopigiwa upatu kuimarisha hali ya walemavu katika siku za
usoni, madaktari huko Italia wameuunganisha mkono huo wa kielektroniki
na neva za mabaki ya mkono wa Dennis uliokatwa baada ya ajali mbaya ya
fataki na hivyo kumwezesha kuhisi kupitia kwa vidole vya mkono huo wa
kielektroniki .
Silvestro Micera aliyeongoza upasuaji huo alifurahishwa mno na uwezo wa mgonjwa wake kuutumia mkono huo bandia .
'' tumeshangazwa sana na urahisi wa mgonjwa wetu
kuwasiliana mara moja na mkono huu bandia wa kielektroniki kuekelea
majukumu ya kushika na kuhisi vitu tofauti . Hata ikiwa upasuaji huu
utakuwa wa muda tu, ninahakika Denis ameotambua mwenyewe kuwa utakuwa
wenye manufaa makubwa kwake katika siku za usoni''
Mkono bandia wa kielectroniki
Dennis hakuficha furaha yake alisema mkono huo umebadilisha kabisa hali yake. ''hisia zangu za mkono zimeimarika maradufu maanake ninawezajua ugumu na mfumo wa kitu chochote ni kama mkono wa kawaida''
Mfumo wa mkono wa Kielektroniki
Habari hii imenukuliwa kama ilivyo kutoka BBC.
|
No comments:
Post a Comment