Tuesday, November 27, 2012

KIJANA UNAETAFUTA AJILA YA POLISI, USALAMA WA TAIFA INAKUUSU SOMA...

Kwa mjibu wa msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja kama Komba ameshakamatwa kuhusiana na kuwepo mtandao mkubwa ndani na nje ya jeshi hilo unajiusisha na kuwalaghai vijana wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi.

Inasemekana vijana zaidi ya 200 walitapeliwa kiasi cha shillingi 800,000/= kila mmoja kwa minajiri ya kuwawezesha kujiunga na Chuo cha Polisi Moshi baada ya kuhonga kitita hicho walitakiwa kulipa tena 25,000/= kama nauli ya kuwafikisha Moshi na kweli mabasi matatu yalikodishwa nakuwafikisha Moshi chuoni.

Baada yakufika chuoni taratibu zote za kuwasajili pamoja na kutakiwa kulipia gharama nyingine za kiasi cha shillingi 50,000/=,walinyolewa vipara na kuanza kupiga kwata kama makuruta wengine.

Kwa mshangao wa vijana hao siku ya pili waliitwa nakuambiwa kuwa wanatakiwa kuondoka hapo chuoni kwa vile sio makuruta halali na hawako kwenye kompyuta za chuo.

Kilichowashangaza zaidi ni pale walipokuwa wanatoka kweye lango la chuo kurudi makwao waliyaona mabasi yale yale yaliyowaleta yakiingia na vijana wengine ambao bila shaka nao wlikuwa wameingizwa mkenge!.

Msemaji wa Polisi ameamewataka wote wenye malalamiko au taarifa kuwa walitoa fedha ili kupatiwa ajira na matapeli hao au mawakala wao kutoa ushirikiano utakaowezesha polisi kukamilisha uchunguzi na kupata ushahidiwa kudhibitisha kesi ya Komba iliyopo mahakamani.

Taarifa zitumwe kwa ujumbe wa mfupi kwa ssimu ya IGP namba 0754785557 au kuwasiliana moja kwa moja makao makuu ya Polisi ghorofa namba 4 Ofisi ya Malalamiko.

No comments:

Post a Comment