Saturday, August 24, 2013

YANGA YAIPIGA ASHANTI 5 KWA 1SIMBA YAVUTWA MKIA...

Pazia la Ligi Kuu ya Vodacom limefunguliwa leo katika viwanja saba tofauti huku katika dimba la Uwanja wa Taifa mabingwa watetezi Young Africans wakiikaribisha timu iliyopanda Ligi Ashanti United kwa kuichapa mabao 5-1 jioni ya leo.

Young Africans inayonolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts imeanza vizuri harakati zake za kutetea Ubingwa kwa kuhakikisha inashinda mchezo wa mwanzo na ndivyo vijana wa Jangwani walivyofanya.

Ilimchukua dakika 10 Jerson Tegete kuipatia Young Africans la kwanza kwa kumchambua mlinda lango wa Ashanti kufuatia pasi nzuri wa winga wa kulia Saimon Msuva kuitoka ngome ya Ashanti na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira wavuni bila ajizi. 

Ashanti walifanya mashambulizi langoni mwa Yanga kupitia kwa Hussein Sued lakini ukuta wa Yanga uliokuwa chini ya Mbuyu Twite na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' ulikuwa kikwazo kwake kumfikia mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez'.

Kiungo Athuman Idd 'Chuji' alitolewa nje dakika ya 18 ya mchezo kuufuaia kuumia na kushinda na kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo Frank Domayo 'Chumvi' . 

Kutokua makini kwa washambuliji wa Yanga Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Jerson Tegete kulizifanya timu kwenda mapumziko zikwa 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kujipatia bao la pili dakika ya 48 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Ashanti na kuachia shuti kali liliokwenda moja kwa moja wavuni.

Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao tatu dakika ya 58 kwa usatdi wa hali ya juu akimalizia pasi safi ya Saimon Msubva aliyewatoka walinzi wa Ashanti United na kujaza krosi safi ambayo Tegete aliiweka kifuani kabla ya kumchambua mlinda mlango.

Yanga iliendelea kucheza inavyotaka huku ikitawala dimba la katikati kupitia kwa viungo wake Haruna Niyonzima, Salum Telela na Frank Domayo hali iliyowapelekea wachezaji wa Ashanti kucheza faulo nyingi na mwamuzi kuwaadhibu kwa kadi za njano na mmoja wao kutolewa nje kwa kadi nyekundu.

Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la nne dakika ya 74 ya mchezo kwa kichwa, akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na mlinzi wa pembeni David Luhende kufuatia Saimon Msuva aliyekuwa amechezewa madhambi na walinzi wa Ashanti United.

Dakika ya 90 Ashanti United walijipatia bao kupitia kwa Shaban Juma kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga waliotegeana kumkaba mfungaji aliyeukokota mpira toka nje ya 18 na kuingia nao ndani ya sita na kumfunga mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez'.

Huku washabiki na wapenzi wa soka wakiwa wanatoka nje wakijua mpira umemalizika, Nizar Khalfani aliipatia Young Africans bao la tano na kukamilisha ushindi huo mnono akimalizia pasi ya Saimon Msuva ambaye leo alikua mwiba mkali kwa walinzi wa Ashanti.

Mpaka dakika 90 za mchezo za mwamuzi Israel Mjuni Nkongo zinamalizika, Young Africans 5 -1 Coastal Union.

Kocha mkuu wa Yanga Ernie Brandts amekipongeza kikosi chake na kusema ni mwanzo mzuri katika msimu huu, aidha amesema wachezaji wake wangekuwa makini basi leo wangeibuka na ushindi mnono zaidi ya hizo bao tano walizozipata kutoka kwa wauza mitumba wa Ilala - Ashanti united.

Mara baada ya mchezo wa leo wachezaji wote wamepewa mapumziko siku ya kesho mpaka siku ya jumatatu watakapoanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union ya Tanga siku ya jumatano tarehe 28.08.2013 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji'/Frank Domayo, 7.Saimon Msuva, 8.Salum Telela, 9.Didier Kavumbagu/Hussein Javu, 10.Jerson Tegete/Nizar Khalfani, 11.Haruna Niyonzima

Wakati huo huo uko Tabora Timu ya Simba imeambulia sare ya magoli 2 kwa 2 na  Rhino rangers na hivyo ni kama imevutwa mkia katika mchezo huo matokeo mengine ni kama hivi 

Mtibwa1 Azam 1

Coastal union2 Jkt Olojolo 0


No comments:

Post a Comment