Wednesday, September 4, 2013

BINTI WA MIAKA 14 AJIFUNGUA WATOTO WATATU BABA WA WATOTO HAO NAE ANAMIAKA 16.

Habari hii inatokea Nchini Kenya ambapo Msichana mwenye umri wa miaka 14  Mwanaharabu Wamukoya kutoka katika kijiji cha  Harambee katika wilaya ya Kakamega amejifungua watoto watatu wote wakiwa ni Wavulana wawili kati yao wamezaliwa wakiwa na uzito wa 1.5 kilogram na mwingine akiwa na uzito wa Kilogram 1.3.Nesi wa zamu katika Hospitali hiyo ya Bugoma Bi,Mary Marumbu alisema Watoto hao pamoja na Mama yao wanaendelea vizuri na wakati wowote wanaweza kuluhusiwa kutoka Hospitalini hapo. Mshangao zaidi ni pale ilipokuja kujulikana kwamba Baba Mzazi wa watoto hao watatu waliozaliwa  bado ni mtoto mdogo kama alivyo Mama yao kwani Baba yao ana Umri wa Miaka 16 ambae pia bado anasoma,Zaidi aliishukuru sana Serikali kwa kuweza kuondoa garama kwa wajawazito wakiwa wanajifungua na ivyo kuweza  kumuwezesha mzazi mwenzie kujifungua pasipo Garama zozote zile.

WITO WETU KWENU TUUNGANE KWA PAMOJA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI,KWA KUTOA ELIMU SITAHIKI NJISI YA KUEPUKA NGONO ZEMBE NA KUTUMIA KINGA PIA.

Unaweza kuitazama video ya binti huyo hapa
www.youtube.com 14 year old girl gives birth to triplets

No comments:

Post a Comment