Saturday, November 23, 2013

"ZITTO KABWE KARIBU CCM TUIJENGE NCHI" MANENO YA JANUARY MAKAMBA

Naibu waziri wa Sayansi na Teknolojia ambae pia anashikilia nyazifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi CCM Mh,January Makamba katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter ameandika ujumbe kwa Mh Zitto Kabwe mara baada ya kamati kuu ya Chama cha Chadema kumvua madaraka yake yote ndani ya chama hicho aliokuwa nayo apo awali na hadi kumfanya kuwa mwanachama wa kawaida baada ya hatua hiyo January Makamba amemuandikia ujumbe Mh,Zitto kama ifuatavyo tunanukuu " kama wenzako hawathamini kazi kubwa uliyofanya kukijenga Chama chenu na kazi unayofanya Bungeni, karibu CCM tuijenge nchi.

hapo chini ndio tweet alioiandika January Makamba;
21 Nov

kama wenzako hawathamini kazi kubwa uliyofanya kukijenga Chama chenu na kazi unayofanya Bungeni, karibu CCM tuijenge nchi.

No comments:

Post a Comment