Monday, September 9, 2013

KAMA KWELI NAIBU SPIKA ULITUMWA ULITUMWA KWA MANUFAA YA NANI?


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), tukio la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuondolewa bungeni mjini Dodoma kwa agizo la Naibu Spika, Bw. Job Ndugai, lilipangwa na Serikali ili kuhakikisha Muswada wa sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba mwaka 2013, unapitishwa bungeni ili kulinda masilahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CHADEMA, Bw. John Mnyika, ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo,Alisema Serikali ilipanga kupitisha muswada huo bungeni ndio maana hata Bw. Mbowe kama Kiongozi wa Upinzani bungeni, aliposimama kutaka kuzungumza, hakupewa nafasi hiyo badala yake alitakiwa akae na alipokataa Bw. Ndugai aliagiza atolewa nje jambo ambalo hawakuliunga mkono.
Aliongeza kuwa, Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wabunge wa CCM wanakuwa wengi katika Bunge la Katiba ili kupitisha mambo wanayoyataka."Kilichopitishwa bungeni na wabunge wa CCM ni kibaya kuliko ilivyokuwa awali...wameharibu zaidi, CHADEMA imepinga kwa masilahi ya makundi mengine ya kijamii ili yaweze kupata uwakilishi katika bunge hilo," alisema.
Bw. Mnyika alisema CHADEMA walipendekeza Bunge la Katiba lipunguze uwakilishi wa chama kimoja ambapo katika kipengele cha wajumbe 166 wanaoteuliwa na rais, iongozwe na kufikia wajumbe 359 lakini Serikali imekataa."Lengo letu ni kutoa nafasi kwa makundi mengine ya kijamii kama wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi na taasisi nyinginezo kutoa wawakilishi wao kwenye bunge hili," alisema.
Alisema upande wa Zanzibar, hakukuwa na wawakilishi waliotoa maoni yao juu ya nafasi ya Zanzibar katika bunge hilo na kilichosemwa na Serikali ni uongo."Serikali baada ya kushindwa kuchakachua Mabaraza ya Katiba, sasa imeona njia pekee ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kwenye Bunge la Katiba wabunge wa CCM wanakuwa wengi," alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Bw. Ndugai kumtoa nje Bw. Mbowe, alisema Naibu Spika amevunja kanuni ya 76 ya Bunge kwani hana nguvu ya kuita askari ambapo kwa mujibu wa kanuni ya 20, alitakiwa kuhairisha shughuli za Bunge."Ndugai amefanya kosa la kuwaingiza watu wasiohusika bungeni na kuruhusu vitendo vya uhalifu vitokee ili kupitisha muswada walioutaka na kulinda masilahi ya chama kimoja.
"Sekretarieti ya CHADEMA itakutana  ili kujadili kwa undani suala hili na kulishughulikia, pia tutatumia nguvu ya umma (wananchi) kuhakikisha katiba haivurugwi, tutakutana na vyama vingine vya upinzani," alisema.Alisema chama hicho hakioni sababu ya kuharakisha katiba badala yake kama wanataka katiba hiyo itumike katika Uchaguzi Mkuu 2015 ni vyema ikaandaliwa ya mpito.
Aliongeza kuwa, katika Bunge lijalo Sheria ya Kura za Maoniambayo itajadiliwa ni ya hatari zaidi kuliko Bunge la Katiba na isipofanyiwa marekebisho, itazusha mgogoro mkubwa zaidi.
Maswali ya kujiuliza hapa kama Watanzania je?ni kweli Naibu spika alitumwa? na kama alitumwa ni kwa faida ya nani na kwa ajili ya nani?je amesahau kiapo alichoapa Bungeni?Kama majibu haya yasipopata majibu basi kunahaja kubwa katiba yetu Spika na Naibu wake wasitokane na chama chochote kile cha siasa bali waombe kulingana na sifa zao na badae chombo kitakachoundwa kwa ajili ya kupitia maombi hayo kiyapitie kwa uwazi kabisa na wananchi wafahamu kabla ya kupitishwa na Bunge.

No comments:

Post a Comment