Wednesday, November 13, 2013

DK MVUNGI AFARIKI DUNIA,PICHA ZA MAPANGA YALIOTUMIKA KUMSHAMBULIA UTAZIONA HAPA PIA.

Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Dk Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.

Wakati huo huo  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid jana jioni (Jumanne, Novemba 12, 2013), Dkt. Sendongo Mvungi arifariki majira ya saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini akiwa katika Hospitali ya Milpark.

"Kwa masikitiko makubwa, Tume inawafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg-nchini Afrika Kusini amefariki dunia leo (Jumanne, Novemba 12, 2013) saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika ya Kusini," amesema Bw. Rashid katika taarifa yake fupi ya awali.

"Taratibu za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Afrika Kusini kuja nchini kwa mazishi zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa leo (Jumatano, Novemba 13, 2013)," ameongeza.

Marehemu Dkt. Mvungi alisafirishwa siku ya Alhamisi, Novemba 7, 2013 kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Katika taarifa yake, Tume pia imewaomba watanzania wote kuungana na familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dkt. Mvungi katika kuomboleza msiba huo.

Picha juu ikimuonyesha Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam SULEIMAN KOVA pamoja na Waziri wa Mambo ya ndani wakionyesha mapanga yaliotumika kumshambulia Marehemu Dk.Mvungi ni matumaini yetu kwa kuwa ushaidi umepatikana na baadhi ya watuhumiwa wamepatikana sasa Tunaomba sheria ichukue mkondo wake kwa unyama huu ili uwe fundisho kwa watu wengine pia wenye tabia kama hizo.

 

PUMZIKA KWA AMANI DK.MVUNGI TUTAKUKUMBUKA DAIMA.


No comments:

Post a Comment