MZEE MANGULA LEO ANAFUNGA NDOA NA KIPENZI CHA MOYO WAKE.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Phillip Mangula
anatarajia kufunga ndoa leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini, mjini Njombe.
Mzee Mangula anafunga ndoa na Mkuu wa Sekondari ya Philip Mangula, iliyopo wilayani Wanging’ombe, mkoani Njombe, Yolanda Kaberege.
Hatua hiyo ya Mzee Mangula kuoa inakuja baada ya aliyekuwa mke wake kufariki dunia mwaka 2004, kutokana na ugonjwa wa saratani.
Msemaji wa familia ya Mzee
Mangula ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) tawi
la Njombe, Dk Lechion Kilimike alilieleza Mwananchi kuwa ndoa hiyo
itaongozwa na Askofu Mstaafu wa Kanisa hilo, Solomon Swalo.
Dk
Kilimike alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda ambaye anatarajia kuwasili kesho mkoani hapa akitokea Mbeya ambako
atatua leo saa 11:00 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Songwe.
Waziri
Mkuu Pinda anatarajiwa kufuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali walioalikwa kwenye
sherehe hiyo.
Habari
zinaeleza kuwa, baada ya kumalizika kwa ndoa hiyo itakayofungwa saa
3:00 asubuhi, Pinda ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za Serikali
bungeni, atakwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti
linaloanza Aprili 9
No comments:
Post a Comment