Thursday, October 3, 2013

JAJI WARIOBA AWAOMBA WANASIASA KUJADILI RASIMU NA SIO KUIJADILI TUME NA WAJUMBE WAKE.

Tume ya Katiba kupitia kwa Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba imefafanua maswala mbalimbali yaliojitokea kutoka wa wanasiasa kuhusiana na Tume hiyo akizungumza Jaji warioba alisema siku zote Tume yake imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na kuwahasa Wanasiasa kujadili Rasimu na siyo Tume au wajumbe wake."Moja ya kazi za kisheria za Tume ni kutoa Elimu kwa Umma na  ni kazi ya wakati wote .Kuhusu kauli ya Mwenyekiti wa Jumuhiya ya Wazazi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Bw, Abdllah Bulembo alioisema hivi kalribuni akiwa jijini Tanga kwamba Tume ya Warioba imeacha kutekeleza majukumu yake na kuingilia Uhuru wa Wananchi wa kutoa Maoni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba alisema ''Sasa naona Bw Bulembo anaona kutoa Elimu ni dhambi"Mwenyekiti huyo alikumbusha kuwa Tume yake imekuwa ikifanya  kazi katika mazingira magumu kutokana na kauli za Wanasiasa lakini inafalijika kwa kauli za wananchi.Nilisema mwishoni mwa mwezi uliopita wanasiasa wamekuwa wakitoa matamshi yaliofanya kazi ya Tume kuwa Ngumu katika mikutano ya Mabaraza ya Katiba.Matamshi mengine yalilenga Tume na wakati mwingine yalinilenga mimi binafsi au hata Wajumbe wa Tume badala ya kuzungumzia Rasimu,Jaji warioba alimalizia kwa kusema Tume yake siku zote imekubali kukosolewa kwa kuamini kuwa kukosolewa ni jambo la kawaida lakini akaongeza kuwa ni vema Wananchi na wanasiasa wakajadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na kuacha kuijadili Tume na Wajumbe wake.




No comments:

Post a Comment