Monday, June 3, 2013

RASIMU YA KATIBA YAZINDULIWA LEO NA HAYA NI MACHACHE YALIOMO!

Rasimu ya Katiba mpya leo imeziduliwa rasimi jijini Dar es salaam ambapo viongozi mbalimbali wameudhulia katika uziduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya karimjee na haya ni mtasali tu wa yale yaliopendekezwa kuwemo kwenye Katiba Mpya.

  • SPIKA NA NAIBU WAKE WASIWE WABUNGE,WALA WASIWE VIONGOZI WA SIASA.
  • UWEPO MUUNDO WA SERIKALI TATU.
  • MAWAZIRI WASIZIDI KUMI NA TANO (15)
  • TUME YA UCHAGUZI IJULIKANE KAMA TUME UHURU YA UCHAGUZI.
  • KUSIWE NA UCHAGUZI MDOGO.
  • KIKOMO CHA KUWA MBUNGE KIWE MIAKA MITATU (3)
  • KATIBU MKUU KIONGOZI KUSIBITISHWA NA BUNGE.
  • MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI WASIBITISHWE NA BUNGE MARA RAIS ANAPOWATEUA.
  • MATOKEO YA URAIS YALUHUSIWE KUOJIWA MAHAKAMANI KAMA MTU ASIPOLIZIKA NDANI YA MWEZI MMOJA MAHAKAMA KUU.
  • MGOMBEA APATE ASILIMIA 50%KUTANGAZWA MSHINDI.
          KUWEPO NA MGOMBEA BINAFSI

Hayo ni baadhi tu ya yale yaliomo sasa hatua inayofata ni Mabaraza ya Katiba kukaa na kuipitia Rasimu hii na kuona kwenye mapungufu kulekebisha kaa tayari kuipata rasimu yote jinsi ilivyo mda mfupi ujao..........!!!!

****************************************************


HOTUBA YA MWENYEKITI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA, JAJIJOSEPH S. WARIOBA, KATIKA MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARIKUHUSU UZINDUZI WA RASIMU YA KATIBA TAREHE 03 JUNI, 2013 KWENYE VIWANJA VYA UKUMBI WA KARIMJEE,DAR ES SALAAM.


Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilali

Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuungano,

Mhe. Mizengo K. P. Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu,

Mhe. Seif Sharif Hamad
Makamu wa Kwanza wa Rais

Serikali yaMapinduzi Zanzibar,

Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (Mb.) - Makamo wa Pili wa Rais - Serikali yaMapinduzi Zanzibar,

Mhe. Mathias Chikawe

Waziri wa Katiba na Sheria,

Mhe. Abubakar Khamis Bakary - Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,

Mhe. Jaji Frederick M Werema - Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania,

Mhe. Othman Masoud Othuman - Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,

Viongozi wa Vyama vya Siasa,

Waheshimiwa Wajumbe wa Tume na Wajumbe wa Sekretarieti yaTume ya Mabadiliko ya Katiba,

Ndugu Wananchi,

Wageni Waalikuwa


Waandishi wa Habari Mabibi na Mabwana.1.0.








UTANGULIZI Ndugu Wananchi,


2
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufikia hatua hii yaleo ya kuzindua Rasimu ya Katiba. pia, niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria halfahii ikiwa ni mwendelezo wa mchakato muhimu wa Mabadiliko ya Katiba ya nchi yetu.Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ilipitishwa Bungeni Novemba, 2011 na kufanyiwamabadiliko Februari, 2012. Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliundwa kwa mujibu waKifungu 6(1) cha sheria hiyo (Cap.83). Wajumbe 34 wa Tume waliteuliwa nakuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,mwezi Aprili, 2012. Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Tume imepewamiezi kumi na minane kukamilisha kazi yake kuanzia siku ilipoanza kazi rasmi ambayoilikuwa Mei 2, 2012.Tume iliandaa ratiba ya utekelezaji wa majukumu yake. Kufuatana na ratiba hiyoTume ilijipanga kukusanya maoni ya wananchi katika kipindi cha miezi mitanokuanzia Mwezi Julai hadi Disemba, 2012. Kazi hiyo ilifanywa kama tulivyopanga.Tume ilijigawa katika makundi na ilitembelea mkoa yote thelathini.
Tume ilifanya mikutano 1,942
ambayo
ilihudhuriwa na wananchi wapatao1,365,337
ambao kati ya hao
wananchi 333,537 walitoa
maoni ama kwamazungumzo ya ana kwa ana au kwa maandishi. Tume pia ilipata maoni yawananchi wengi, wa ndani na nje ya nchi kwa njia mbali mbali kama vile; Mikutanoya hadhara, Fomu maalum za Tume, barua kupitia Masanduku ya Barua ya Tume,Mitandao ya Kijamii ya barua pepe; facebook ya Tume, Tovuti ya Tume; Makalambalimbali kutoka kwenye magazeti na ujumbe mfupi wa simu.Tume ilitumia mwezi Januari, 2013 kukusanya maoni ya makundi mbali mbali katika jamii, ikiwa ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi za Serikali, taasisi za dini,wakulima, wafugaji, wafanyakazi, asasi za kiraia na kadhalika.
Makundi zaidi ya160
yalikutana na Tume na kutoa maoni. Tume pia ilipata maoni ya viongozi wa juuwa Serikali walioko madarakani na waliostaafu.
Kwa jumla viongozi 43walitoamaoni.

Tume ilipanga kutumia miezi mitatu ya Februari, Machi na Aprili kuchambua maoni yawananchi na kuandaa Rasimu ya Katiba. Lakini tuligundua kwamba maoni tuliyopatayalikuwa mengi sana, na pamoja na matumizi ya teknolojia ya kisasa, tulitambuaumuhimu wa kuongeza muda hadi mwisho wa mwezi Mei, Maoni ya wananchiyaligusa mambo yote yanayohusu Katiba na mengi ya maoni hayo yalikinzana. Aidha,baadhi ya maoni yaligusia masuala ya Kisera, Kisheria na Kiutendaji. Tulifanyauchambuzi makini na wa ndani wa maoni hayo na kazi hiyo tumeikamilisha na rasimuimeandaliwa na Tume na leo tupo hapa kwa ajili ya kuizindua, ambapo Wananchiwatapata nafasi ya kuisoma. Kwa leo, kwa niaba ya Tume, napenda kutaja maeneomachache tu ambayo tunayapendekeza.

2.0.

IBARA ZINAZOPENDEKEZWA KWENYE RASIMU YA KATIBANdugu Wananchi,
Katiba yetu ya sasa
ina ibara 152.
Tume ilifanya jitihada kubwa sana kuandaarasimu ambayo siyo ndefu. Lakini katika hali halisi haikuwezekana.
Rasimu yaKatiba tunayopendekeza ina ibara 240
.
3.0.

MISINGI MIKUU YA TAIFA
Utangulizi wa Katiba ya sasa ndio unaobeba misingi mikuu ya Taifa ambayo ni
Uhuru, Haki, Udugu na Amani
. Tume inaamini kwamba misingi hii ni mizito nainastahili kubaki kwenye Katiba mpya. Hata hivyo, Tume imeona ni busara kuongezamisingi mingine mitatu ya Usawa, Umoja na Mshikamano. Hivyo, Tumeimependekeza Katiba iwe na Misingi Mikuu saba ya Taifa;yaani;
Uhuru, Haki,Udugu, Usawa, Umoja, Amani na Mshikamano.4.0.

TUNU ZA TAIFA
Katiba yetu ya sasa haina sehemu inayoelezea tunu za Taifa (National Values).Wananchi wengi walitoa maoni kwamba Katiba itaje Tunu za Taifa. Tumeimependekeza Tunu zifuatazo zitajwe ndani ya Katiba.
Tunu hizo ni;- Utu




4

Uzalendo, Uadilifu, Umoja, Uwazi, Uwajibikaji na Lugha yetu ya taifa yaKiswahili.

5.0.

MALENGO YA TAIFA
Tume ilipozunguka nchi nzima wananchi walizungumzia sana kuhusu malengo yataifa. Walitaka Katiba ionyeshe dira ya taifa. Wananchi wanayo ndoto yao yaTanzania ya kesho na kesho kutwa. Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, kuna suranzima inayohusu Malengo mahsusi na ya msingi ya mwelekeo wa shughuli zaKiserikali na Sera za Kitaifa. Rasimu ya Katiba inaeleza kuwa
Malengo ya Kitaifa yaliyoainishwa ndani ya Rasimu yatakuwa ni Mwongozo kwa Serikali,Bunge, Mahakama, Vyama vya Siasa, Taasisi na Mamlaka nyingine, na kwakila mwananchi katika matumizi au kutafsiri Masharti ya Katiba au Sherianyingine za Nchi
.Kwa msingi huo, Tume imependekeza malengo makuu ya taifa yapanuliwe kwampangilio wa


kuonesha malengo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni,kimazingira na sera ya mambo ya nje
. Malengo hayo yameingizwa kwenyeRasimu ya Katiba.
6.0.

VYOMBO VYA KIKATIBA
Wananchi walizungumzia suala la kubainishwa kwa vyombo vya Kikatiba nakuingizwa kwenye
Katiba ili viwe na nguvu ya Kikatiba katika utekelezaji wamajukumu yao.
Tume imependekeza baadhi ya vyombo vifuatavyo viwe vyaKikatiba; Tume ya Uhusiano na Uratibu wa Serikali, Baraza la Mawaziri, KamatiMaalum ya Makatibu Wakuu na Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri; Baraza la Ulinzi naUsalama la Taifa, Tume Huru ya Uchaguzi, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Tumeya Utumishi wa Umma, Tume ya Maadili ya Uongozi na Uwajibikaji, Tume ya Haki zaBinadamu na


Utawala Bora


7.0.

MAADILI YA VIONGOZI NA MIIKO YA UONGOZI
Wananchi wengi pia walizungumzia kwa upana sana kuhusu maadili na miiko ya Viongozi, kwa kuzingatia maoni ya wananchi
Tume inapendekeza maadili yaviongozi wa umma, pamoja na miiko ya uongozi yawekwe kwenye Katiba.
Tume pia imependekeza kuwa
Sekretariati ya Maadili ibadilishwe kuwa Tume yenye mamlaka makubwa ya kusimamia maadili ya viongozi wanaovunjamiiko ya uongozi.8.0.

HAKI ZA BINADAMU
Kuhusu haki za binadamu wananchi walitaka haki hizi ziimarishwe na kusiwe navikwazo visivyo vya lazima. Tume imependekeza mabadiliko katika baadhi ya haki zabinadamu kwa madhumuni ya kuziimarisha. Moja ya mabadiliko hayo ni
kuhusu
uhuru wa mwananchi kushiriki shughuli za umma. Tume inapendekeza kwambavikwazo vilivyowekwa kuzuia mgombea huru viondolewe. Kwa maana nyingine
Tume inapendekeza mgombea binafsi aruhusiwe.
Tume pia
, inapendekeza haki mpya ziingizwe kwenye Katiba
ikiwa ni pamojana haki ya wafanyakazi, , haki ya mtoto, haki za Watu wenye Ulemavu, Haki zaWanawake, Haki za Wazee, Haki za Makundi Madogo katika Jamii, Haki ya Elimu naKujifunza, Haki ya kupata habari, Haki na uhuru wa habari na vyombo vya habari nakadhalika.
9.0.

URAIA
Wananchi wengi walipendekeza kuwa suala la Uraia libainishwe wazi kwenye Katiba.Tume imependekeza kwa kutaja Raia wa Jamhuri ya Muungano na haki zake.
10.0.

MIKOPO NA DENI LA TAIFANdugu Wananchi,
Wananchi walizungumzia suala la uwepo wa Ukomo wa nchi kukopa na uwepo wautaratibu wa kulipa Deni la Taifa ili kuilinda Nchi isiwe na deni kubwa. Kwa kuzingatia


maoni ya Wananchi, Tume imependekeza kuwa, Serikali itawajibika kutoa taarifaBungeni kuhusu Mikopo kwa kuainisha kiasi cha deni lililopo, riba yake na matumiziya fedha za Mikopo na utaratibu wa kulipa Madeni ya Taifa.
11.0.

MFUMO WA UTAWALA
Kuhusu utawala, Tume inapendekeza Tanzania iendelee na mfumo wa Jamhuri kwamaana ya nchi inayoongozwa na Rais Mtendaji ambaye ni Mkuu wa nchi, Kiongozi waSerikali na Amiri Jeshi Mkuu.

12.0.

UCHAGUZI WA RAIS

12.1.

Umri wa kugombea Urais
Tume ilipokea maoni yanayokinzana kuhusu umri wa mwananchi kugombeaUrais. Baadhi walipendekeza mtu akishakuwa na sifa ya kupiga kura awe pia nasifa ya kugombea Urais. Umri wa mtu kuruhusiwa kupiga kura ni miaka 18.Wengine walipendekeza umri uliopo kwenye Katiba wa mtu kugombea Urais,yaani kuanzia miaka 40 na kuendelea, uendelee kubaki kama ulivyo.Wengine walisema Umri wa mtu kuruhusiwa kugombea Urais uwe miaka 35 aumiaka 50 na kuendelea.Tume imeyachambua maoni yote hayo, ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba zaNchi zingine na uhalisia wa watu wanaogombea na kuchaguliwa kuwa Maraiskatika Nchi mbalimbali Duniani ambazo zingine zimeruhusu wagombea wa nafasiya Urais kuwa na umri chini ya miaka 40.

Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na umri wa miaka40 au zaidi.
Kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na hali halisi, Tume inapendekeza Raisaendelea kuchaguliwa na wananchi na pamoja na sifa nyingine, mtu anayeombaurais asiwe chini ya miaka 40.


Uchaguzi wa Rais itakuwa kama ilivyo sasa, yaani mgombea Urais atakuwa namgombea mwenza kwa utaratibu kama ilivyo sasa. Isipokuwa, Tumeimependekeza

Mgombea Urais anaweza kupendekezwa na Chama chaSiasa au kuwa Mgombea Huru
.
Mgombea wa nafasi ya Rais atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwaamepata kura zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Hata hivyo,
matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwaMahakamani,
lakini siyo kila mtu anaweza kufungua kesi. Wanaowezakufungua kesi ni wagombea Urais. Aidha, ni Mahakama ya Juu pekee ndiyoitakuwa na Mamlaka na uwezo wa kusikiliza malalamiko kuhusu matokeo yauchaguzi wa Rais na shauri lazima liamuliwe ndani ya mwezi mmoja, yaani sikutherathini.
Rais aliyeshinda ataapishwa siku thelathini tangu alipotangazwa kuwamshindi au kuthibitishwa na Mahakama
.
13.0.

MADARAKA YA RAISNdugu Wananchi,
Tume inapendekeza kwamba, Rais abaki na madaraka ya uteuzi wa viongozi wangazi za juu. Hata hivyo inapendekezwa Rais ashirikiane na taasisi na vyombovingine katika uteuzi. Kwa mfano:
Uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri
, Rais atateua na Bunge litathibitisha.
Kuhusu Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu
Rais atawateua kutokana na majina yawatu waliopendekezwa na Tume ya Uutumishi wa Mahakama na baada ya hapoBunge litathibitisha.
Kuhusu Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama
inapendekezwa kianzishwechombo kipya kitakachoitwa Baraza la Ulinzi na Usalama la Taifa, ambalo kati ya

majukumu yake itakuwa ni kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Wakuu wa vyombo vyaulinzi na usalama.
Kuhusu Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu
watateuliwa na Raiskutokana na mapendekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma.

14.0.


KINGA YA RAIS
Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kamailivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa.

15.0.

IDADI YA MAWAZIRI
Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na
Mawaziri wasiozidi kumi natano
na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bungeisipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.

16.0.

BUNGE

Ndugu Wananchi,
Kuhusu Bunge kutakuwa na wabunge wa aina mbili. Kutakuwa na
Wabunge wakuchaguliwa
na
wabunge watano wa kuteuliwa
na Rais kuwakilisha Watuwenye Ulemavu.
Kila Jimbo la Uchaguzi litakuwa na Wabunge Wawili mmoja mwanamke namwingine mwanamume.

Tume inapendekeza kwamba, Mbunge akifukuzwa na Chama cha Siasa abaki kuwaMbunge lakini akihama Chama atapoteza Ubunge wake.Inapendekezwa ukomo wa Ubunge uwe vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Hatahivyo,
wananchi wanaweza kumwondoa mbunge wao kabla ya mwisho wakipindi chake.
Inapendekezwa pia
kusiwepo na uchaguzi mdogo
isipokuwa kama nafasiinayokuwa wazi inatokana na Mbunge huru ndipo utafanyika uchaguzi mdogo kujaza

nafasi hiyo, lakini kama nafasi ikiwa wazi kutokana na Mbunge wa Chama cha Siasabasi nafasi hiyo, ijazwe na mtu kutoka Chama hicho.

Inapendekezwa Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasiwe Viongozi wa vyama vya Siasa.

17.0.

TUME YA UCHAGUZI
Tume imefanya uchambuzi wa maoni ya wananchi kuhusu Tume ya Uchaguzi. Tumeinapendekeza jina la tume liwe
Tume Huru ya Uchaguzi.
Tume pia inapendekezasifa za wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ziwekwe kwenye Katiba. Wajumbe waTume Huru ya Uchaguzi watapatikana kutoka miongoni mwa watu wenye sifazilizoainishwa ndani ya Katiba kwa kuomba. Majina ya waombaji yatachambuliwa naKamati ya Uteuzi ambayo Mwenyekiti wake atakuwa Jaji Mkuu na wajumbe wenginesita ambao ni Majaji Wakuu wa nchi Washirika, Spika wa Bunge la Jamhuri yaMuungano, Maspika wa Mabunge wa nchi Washirika na Mwenyekiti wa Tume ya Hakiza Binadamu.Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateuaMwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuziwao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe watume ya uchaguzi.

Inapendekezwa Tume huru ya Uchaguzi isimamie masuala ya uchaguzi,kura ya maoni na Usajili wa Vyama vya Siasa.

18.0.

MAHAKAMA
Kuhusu Mahakama inapendekezwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Juu (SupremeCourt) Majaji wa Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani watateuliwa na Raisbaada ya kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

19.0.

MUUNDO WA MUUNGANO


10
Ndugu Wananchi,
Suala la muundo wa Muungano
ndilo lililokuwa gumu kuliko masuala yote.
Tume ilitumia muda mwingi kuchambua maoni ya wananchi. Pamoja na kwambahadidu za rejea zilielekeza Tume kuzingatia uwepo wa Muungano, baadhi yawananchi walitoa maoni kwamba Muungano uvunjwe na Tume iliyapokea maonihayo. Licha ya kwamba waliotaka kuvunjwa muungano walikuwa wachache sana,Tume ilichambua sababu walizotoa na kuridhika kwamba hazikuwa na uzito.Wananchi walio wengi walitaka Muungano uendelee. Kati yao wapo waliopendekezaMuungano wa Serikali moja, Serikali mbili, Serikali tatu, Serikali nne na muungano wamkataba. Sababu za wale waliopendekeza Serikali nne hazikuwa na uzito, kwa hiyoTume ikaamua kutopendekeza muundo huo.Wananchi waliopendekeza Serikali moja walikuwa wachache lakini sababu zaozilkuwa na uzito. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia hali halisi iliona ni changamotokubwa kuwa na Muungano wa Serikali MojaWananchi waliopendekeza Muungano wa Mkataba walikuwa wengi (hasa wananchiwa Zanzibar) na sababu zao zilikuwa na uzito. Lakini uchambuzi wa Tume ilionekanawazi kwamba ili kupata mkataba lazima kwanza kuwe na nchi mbili huru kabisa lakinihakukuwa na mazingira ya uhakika ya kupata mkataba wa muungano. Tume ilionakuna changamoto ya muungano kuvunjika ingawa waliotoa maoni walisisitizamuungano ubaki. Hivyo, Tume iliamua kutopendekeza muundo huo.Wananchi waliopendekeza Tanzania iendelee na Muundo wa sasa wa Serikali mbiliwalikuwa wengi na sababu zao zilikuwa nzito. Hata hivyo, wananchi katika kundi hiliwalipendekeza mabadiliko mengi na makubwa. Tathmini ya Tume ilionyeshakwamba isingewezekana kufanya mabadiliko yote yaliyopendekezwa.Wananchi waliopendekeza muundo wa Serikali tatu walikuwa wengi kuliko makundiyote. Sababu zao zilikuwa nzito lakini pia kulikuwa na changamoto nyingi na nzito.Pamoja na maoni ya wananchi Tume ilirejea sababu za kupendekeza muundo huuzilizotolewa na Tume zilizopita na Tafiti zilizofanywa na Tume kuhusu aina mbalimbal
I

za Muungano. Baada ya yote hayo Tume ilifikia uamuzi wa kupendekeza
mfumo waSerikali tatu.

Yaani Serikali ya Shirikisho, Serikali ya Tanzania Bara naSerikali ya Mapinduzi Zanzibar.20.0.

ORODHA YA MAMBO YA MUUNGANONdugu Wananchi,
Tume imependekeza katika Rasimu ya Katiba kuwa orodha ya Mambo ya Muungano
yawe 7 badala ya 22 yaliyopo sasa.
Mambo ya muungano yanayopendekwa ni:
1.Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2.Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
3.Uraia na Uhamiaji
4.Sarafu na Benki Kuu
5.Mambo ya Nje
6.Usajili wa Vyama vya Siasa
7.Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya


Muungano.

21.0.

BENKI KUU
Kwa kuwa Tume imependekeza Muungano wa Shirikisho kutokana na uzito wa maoniya wananchi. Hivyokutakuwa na Benki Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaitakayokuwa na
wajibu wa kusimamia masuala ya Sarafu na Fedha za Kigenina Benki za Washirika wa Muungano
.


12
22.0.

BENKI ZA SERIKALI ZA WASHIRIKA
Kutokana na pendekezo la kuwepo kwa Serikali ya Shirikisho la Nchi tatu,inapendekezwa kuwepo kwa Benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti yafedha za Serikali za kila Mshirika wa Muungano na kuzisimamia benki za biasharakatika mamlaka zao.
23.0.

BAADHI YA MAMBO AMBAYO HAYAMO KWENYE RASIMU YA KATIBA

23.1.

Serikali ya MajimboNdugu Wananchi,
Tume ilipokea maoni kuhusu mambo mengine muhimu ambayo hayamo katikarasimu hii. Moja ya mambo hayo ni
Serikali za Majimbo
. Tume ilichambuamaoni na sababu za wananchi kupendekeza Serikali za Majimbo lakini Tumeilibaini changamoto nyingi na ikaamua kutopendekeza muundo huu.Kwanza,
baada ya kuamua kupendekeza Muundo wa Muungano waSerikali Tatu
, ilionekana ni dhahiri kuongeza ngazi nyingine ya Serikali ingeletagharama kubwa. Serikali nyingine kumi zingekuwa na Wakuu wa Majimbo,Mabaraza ya Mawaziri na Mabunge na
gharama yake ingekuwa kubwa.
Pili, katika kutembelea nchi Tume ilishuhudia
dalili za wazi za mivutano yaUdini, ukanda,malalamiko ya upendeleo wa baadhi ya maeneo naukabila
. Dalili zilikuwa wazi kwamba
utawala wa majimbo ungeirudishanchi kwenye utawala utakaoigawa nchi kwa misingi ya ukabila, udinina ukanda na kuzigawa rasilimali za taifa kikanda na hivyo kuletatofauti kubwa ya kimaendeleo katika nchi.23.2.

Mahakama ya KadhiNdugu wananchi,
Jambo la pili ni mahakama ya kadhi. Tume ilipokea maoni mengi kuhusu sualahili. Baadhi ya wananchi walitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba na


wengine walipinga. Baada ya kuamua kuwa Muundo wa Muungano uwe waSerikali Tatu,
Tume iliona kuwa Mahakama ya Kadhi siyo suala laMuungano
na imeliacha ili
lishughulikiwe na Washirika wa Muungano.
Hata hivyo ilionekana kuwa suala
siyo kuwapo au kutokuwapo
kwamahakama ya kadhi.
Mahakama hizo zinaweza kuwapo bila ya kuwakatika Katiba
. Zanzibar kuna mahakama ya kadhi bila kuingizwa kwenyeKatiba ya Zanzibar. Kwa kutumia uzoefu huo hata Tanzania Bara inawezakupata ufumbuzi wa suala hili.
23.3.

Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa WilayaJambo la Tatu ni Kuwepo au kutokuwepo kwa Wakuu wa Mikoa naWilaya
. Baadhi ya Wananchi walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiwepo,wengine walitaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kuwepo lakiniwachaguliwe na wananchi na waengine wakasema wawepo na waendeleekuteuliwa na Rais kama ilivyo sasa. Tume ilitafakari kuhusu suala hili na kuamuakwamba siyo suala la Muungano na kwa kuwa Muundo wa Muunganoimependekezwa uwe wa Serikali Tatu,
Tume iliona suala la uwepo aukutokuwepo na namna ya upatikanaji wa Wakuu wa Mikoa na Wilayalishughulikiwe na Washirika wa Muungano.23.4.

Serikali za MitaaKuhusu Serikali za Mitaa,
Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusukuziimarisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzipatia uhuru kamili wakujiamulia mambo yao bila kuingiliwa na Serikali Kuu. Tume ilitafakari suala hilina kuamua kwamba siyo jambo la Muungano na hivyo,
litashughulikiwakwenye Katiba za Washirika wa Muungano.23.5.

Uraia wa Nchi mbiliNdugu Wananchi



14
Jambo la tatu ni Uraia wa Nchi mbili. Tume ilipokea maoni kutoka kwa wananchimbalimbali kuhusu kuwekwa kwenye Katiba suala la Uraia wa nchi mbili. Baadaya kufanya uchambuzi kwa kutengenisha mambo yapi ni ya Kikatiba na yapiyanaweza kutekelezwa bila kuingizwa kwenye Katiba bali kwenye Sheriainayohusu jambo husika,
Tume imependekeza kuwa suala la Uraia wa nchimbili linaweza kuwekwa kwenye Sheria badala ya kuwekwa kwenyeKatiba
. hii ni kwa sababu kutokana na utafiti uliofanywa na Tume, suala hilolinaweza kubadilika wakati wowote na hivyo likiwa kwenye Katiba linawezakuifanya Katiba kubadilishwa mara kwa mara.
24.0.

MWISHO
Naomba nichukue fursa hii kwa niaba ya Tume kuwashukuru Watanzania wote kwakushiriki kikamilifu katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba, kuanzia hatua ya kutoamaoni na kuwachagua wawakilishi wenu watakaopata fursa ya kuipitia, kuijadili nakuitolea maoni Rasimu ya Katiba. Ushirikiano huu ulikuwa muhimu sana kwa Tumeya Mabadiliko ya Katiba hasa ukizingatia kuwa lengo ni kupata Katiba Mpya ambayoitaakisi ndoto na matakwa ya Wananchi wa Tanzania.Tume ya Mabadiliko ya Katiba, inatoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:1.

Kwa kuipatia vifaa afisi na mahitaji ya lazima2.

Kwa kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu,3.

Kwa
kutokuingilia Uhuru wa Tume
wakati wa Utekelezaji wa Majukumuyake na4.

Kutoa
Wataalam wenye Weledi, Mahiri, Makini na Waadilifu
ambaowameunda Sekretarieti ya Tume.
Ndugu Wananchi

Shukrani za pekee ziwaendee:1.

Wakuu wa Mikoa,2.

Wakuu wa Wilaya,3.

Wakurugenzi / Makatibu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa,4.

Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Wilaya,5.

Watendaji wa Kata, Vijiji, Mitaa na Masheha.Kwa kuisaidia Tume kutekeleza Majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, tunazishukuru Asasi za Kiraia, Taasisi, Jumuiya za Kidini, Vyama vya Siasa na Makundi mbalimbalikwa namna walivyoshiriki katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika kutoa maoni.Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu, Tunawashukuru Wanahabari wote kwa kazi nzuriwaliyoifanya ya kuisaidia Tume kufikisha taarifa mbalimbali za Tume kwa Wananchi nakatika kuhamasisha Wananchi kushiriki katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.Nachukua nafasi hii kuwaomba Wananchi kupitia Mabaraza ya Katiba ya Wilaya,Mabaraza ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye Malengo yanyofananakushiriki vyema, kwa umakini, utulivu na kwa amani katika hatua hii ya kuipitia,kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba.Tume imekuwa ikithamini na itandelea kuthamini mawazo na maoni kutoka kwaWatanzania wote.Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
www.katiba.go.tz SASA NAKUOMBA MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS UIZINDUE RASMIRASIMU YA KATIBA
Ahsanteni kwa kunisikiliza

No comments:

Post a Comment