Picha inayoonekana kwenye Gazeti la Nipashe ni majeruhi aliejeluhiwa katika tukio hilo akiwa amelazwa hospitalini.
MWANAFUNZI
wa Chuo cha Ufundi (VETA), mkoani Dodoma, Taliki Juma (22), amefariki
dunia baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli. Mbali na mwanafunzi
huyo kufariki, watu wengine wanane waliokuwa karibu na moto huo nao
walijeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na
kusainiwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa, David Misime, tukio hilo
lilitokea juzi saa 12.30 jioni katika Kitongoji cha Machaka, Kata ya
Nzughuni.
Kamanda Misime alisema, katika tukio hilo marehemu alinunua mafuta ya
petroli lita tano katika kituo cha mafuta cha Nanenane na kisha
kujilipua.
“Juma ambaye ni mwanafunzi wa fani ya ufundi wa magari, alimwaga petroli hiyo ndani ya saluni ya Irene Mapunda na kujilipua.
“Watu waliokuwa karibu naye walijaribu kumsihi asijilipue lakini
hawakufanikiwa, kwani aliwasha kibiriti ndani ya saluni hiyo na
kusababisha moto mkubwa kulipuka ambao uliwaunguza wengine waliokuwa
karibu naye pamoja na mali zote zilizokuwa ndani ya Saluni hiyo.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa
kimapenzi, hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linaendelea na
uchunguzi wa kina juu ya tukio hili,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliojeruhiwa ni Mugina Hessein (32), Benson
Mushi (11) Japhet Japhet (18), Meshack John (18), Swaibu Kassim
(20),Ester Silau (30), Shaban Pili (20) na Fedrick Gabriel (21).
Majeruhi wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) na
tathimini ya hasara iliyosababishwa na moto huo bado haijafahamika.
|
No comments:
Post a Comment