Wednesday, August 14, 2013

CCM IMEWAFUKUZA UWANACHAMA NA KUWAVUA UDIWANI MADIWANI 8.

Ule mgogoro uliokuwa ukiendelea katika Manispaa ya Bukoba kati ya Baadhi ya madiwani na Meya wa manispaa hiyo Mh,Anatory Aman ambapo madiwani wachama cha mapinduzi CCM walikuwa wakimlalamikia kuwa hawashilikishi kwenye baadhi ya mambo yanayoendelea katika manispaa hiyo ya Bukoba kama madiwani.Ikumbukwe kwamba Madiwani hao waligomea kikao kilichoitishwa kwa lengo la kupitisha Bajeti ya 2012/2013 baada ya kuhudhuliwa na madiwani 11 kati ya 24 na kumpelekea Mkurugezi wa Halmashauli kwa mujibu wa sheria kutoa siku 7 kurejewa kwa kikao hicho lakini pia Baadhi ya madiwani waligoma tena kuhudhulia na kwa hatua hiyo ingeweza kusababisha Kuvunjwa kwa Halmashauli hiyo na pamoja na juhudi mbalimbali kufanyika kusuruhisha mgogoro huo kwa viongozi wa juu wa Chama akiwemo Makamu mwenyekiti mzee Mangula na hivi karibuni Rais na Mwenyekiti wa chama Taifa Mh Jakaya Kikwete kugonga mwamba hatimaye,

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amesema kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutokana na mgogoro uliokuwa ukiendelea.

Waliofukuzwa ni:

1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph Ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho) na ikumbukwe kwamba

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo

1.Kashai-Amefukuzwa

2. Miembeni-Amefukuzwa

3.Miembe-Amefukuzwa

4.Nyanga-Amefukuzwa

5.Hamugembe-Amefukuzwa

6.Kitendaguro-Amefukuzwa

7.Ijuganyondo-Amefukuzwa

8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)

9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)

10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)

11.Bilele-Amebaki(CUF)

12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)

13.Bakoba-Amebaki(CUF)

14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA)


No comments:

Post a Comment