Hama
kweli sasa sijui ndo Maendeleo yanazidi katika Dunia hii au ndo haki
inafuatwa wakati baadhi ya Nchi zao la Bangi linapigwa marufuku na
uvutaji wake pia ni kosa lakini hali ni tofauti katika nchi ya Uruguay
baada ya hivi majuzi Bunge la nchi hiyo kupitisha
muswada wa sheria wa kuidhinisha matumizi ya bangi.Kutokana na
kura zilizopigwa bungeni,kati ya wabunge 94,wabunge 50 wamepiga kura ya
kukubali matumizi ya bangi.
Sheria hiyo inaonyesha kwamba serikali pekee ndiyo itakayosimamia na
kufungua na kumiliki maduka hayo kwasababu wafanya biashara binafsi
wamekua wakiuza 'kijiti'hicho kwa bei ya juu na kupata faida kubwa na
kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wake.
Pia sheria hiyo inasema kwamba wageni hawataruhusiwa kununua bangi hiyo
na kila mteja anatakiwa kua na kitambulisho kinachoonyesha uraia wake na
umri wake,na pia wateja wote watakua wakiolozeshwa kwenye daftari
maaulumu kwa ajiri ya kutoa bonus kwa mteja aliyenunua mara nyingi!!!
Kitendo hicho cha kupitisha mswada huo kimeufanya Umoja wa Mataifa washutumu hatua hiyo.
|
No comments:
Post a Comment