Joshua Mulundi
(21) raia wa Kenya aliyekuwa anatuhumiwa kumteka na kumtesa Dk Ulimboka
na baadaye kuachiwa huru na mahakama na baadaye kufunguliwa kesi ya
kulidanganya jeshi la polisi, ahukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela ama
kulipa faini ya shilingi elfu moja (1000) baada ya kukili kosa lake.
Hata hivyo mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini hiyo na hivyo kuachiwa huru.Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi Aloyce Katemana baada ya wakili wa serikali kusoma maelezo ya mshitakiwa kwamba alikili kutoa taarifa za uongo kwa jeshi la polisi.Kabla ya hukumu hiyo kutolewa mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa ilo ni kosa lake la kwanza kulifanya.Pia alijitetea kuwa Juni 27, 2012 akiwa Arusha alitekwa na
kupelekwa Dar es Salaam ambako alikuwa hana mwenyeji wala hakuwahi
kufika.
Alisema kutokana na kutekwa huko alichanginyikiwa
hivyo kukubali chochote alichoambiwa afanye kwa kuwa aliyemteka alikuwa
na silaha na alimwelekeza mambo ya kuzungumza.
“Mheshimiwa kwa ajili ya vitisho hivyo, nilikwenda
Kawe katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililoko kwenye eneo la
Tanganyika Packers, mbele ya Mchungaji Joseph Malwa Kiliba na kuungama
kuwa ni miongoni mwa watu waliomtesa Dk Ulimboka katika Msitu wa Pande,”
alisema Mulundi na kuongeza:
“Siwalaumu Serikali, upande wa mashtaka wala polisi kwa kitendo cha kuniweka gerezani kwa muda mrefu, najilaumu mimi mwenyewe.”
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Kweka aliiambia
Mahakama kuwa hana kumbukumbu za uhalifu za mshtakiwa lakini aliomba
apewe adhabu kali kutokana na mazingira ya tukio hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Katema alisema alifikia uamuzi huo kwa kuzingatia maombi ya mshtakiwa ya kupunguziwa adhabu.
|
No comments:
Post a Comment